
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Mfaranyaki, Ruvuma wakifurahia jambo.
*************
Hatua hiyo inatokana na kubaini kuwa ni asilimia 23 tu ya Watanzania nchini ndio waliosajiliwa na kupewa vyeti vya kuzaliwa.
Akizungumza
wakati wa uzinduzi wa Mpango huo kwa Manispaa ya Ilala Dar es Salaam
jana, Meya wa Manispaa hiyo, Jerry Silaa, alisema utasaidia kuongeza
idadi ya Watanzania wenye vyeti vya kuzaliwa ambavyo ni tiketi ya kupata
mahitaji muhimu na kutambulika kama wazawa wa nchi.
“Asilimia 23 ni
ndogo sana, hasa ikizingatiwa kuwa vyeti vya kuzaliwa ni nyaraka muhimu
kwa raia yeyote, ili apate mahitaji muhimu nchini mwake kama vile hati
ya kusafiria, kusoma, kitambulisho cha uraia na hata haki ya kupiga
kura,” alisema Silaa.
Alisema mpango huo ambao unaanzia Ilala utaanza
na shule za msingi za Serikali ambapo watoto wasiokuwa na vyeti hivyo,
kupitia walimu waliopewa mafunzo maalumu ya usajili na utoaji vyeti
hivyo, watasajiliwa na kuvipata ndani ya wiki moja.
Hata hivyo,
alionya walimu waliochaguliwa kushughulikia usajili huo, kuhakikisha
kuwa wanatanguliza uzalendo na kusajili na kutoa vyeti kwa watoto ambao
wamehakikiwa na kuthibitika kuwa ni Watanzania na si vinginevyo.
“Napenda
kueleza, kwamba kumekuwa na changamoto ya kukosa uaminifu kwa watendaji
wengi wa Serikali, ambao wanaaminiwa kukusanya fedha. Nasisitiza kwamba
fedha ya Serikali ni lazima iwasilishwe inakotakiwa kwa njia sahihi.
“Naamini
walimu mtakuwa waaminifu na atayefanya kinyume, sheria itachukua mkondo
wake. Naamini walimu wa Manispaa yangu hamtaniangusha katika hili,”
alisisitiza.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Rita, Philipo
Saliboko, alisema katika kutekeleza mpango huo, Wakala huyo ameamua
kushirikisha walimu na waratibu katika usajili na uhakiki wa watoto hao
ambapo hatua ya mwisho itafanywa na watendaji wa Rita kwa kuhakiki
taarifa za watoto hao na kutoa vyeti.
“Awamu ya kwanza ya mpango huu,
tumeamua kuanzia Dar es Salaam, katika manispaa ya Ilala, na itafutiwa
na Kinondoni na kumalizikia Temeke. Katika mikoa mingine bado mchakato
wa kifedha unaendelea ili kuendelea na mpango huu,” alisema Saliboko.
Alisema
Ilala jumla ya walimu 105 na waratibu 28 ndio watashiriki kusajili
watoto hao kwa kuzungumza na wazazi wao na kuhakiki taarifa zao kabla ya
kuziwasilisha Rita kwa uhakiki zaidi na kuchapishwa kwa vyeti hivyo.
Akizungumzia
shule za msingi na sekondari binafsi, Saliboko alisema watatumia walimu
waliopewa mafunzo, lakini pia watashirikisha taasisi muhimu kama
Uhamiaji ili kutotoa vyeti kwa watoto wasio wazawa wa Tanzania
Post a Comment