
Wizara ya mambo ya ndani ya nchi
ya Misri imesema kuwa inachunguza maneno yanayoandikwa kwenye mitandao
ya kijamii yakiwa na kitambulisho, yaani "hashtag", yanayomtusi waziri
wa ulinzi aliyestaafu ili kugombea urais, Field Marshall Abd-el-Fattah
el-Sisi.
Heshtegi hiyo ambayo tafsiri yake ni "mpigie
kura kuwadi", imesambazwa kwenye Twitter zaidi ya mara 100-milioni na
imependwa na watu zaidi ya 40,000 kwenye Facebook.Inaarifiwa kuwa wizara ya mambo ya ndani ya Misri imesema itawakamata watu wanaoitumia sana heshtegi hiyo.
Maneno hayo piya yamekuwa yakichorwa kwenye kuta za mjini Cairo chini ya mabiramu ya picha za Bwana Sisi.
Field Marshall E-Sisi aliipindua serikali iliyochaguliwa kwa njia za kidemokrasi ya Mohamed Morsi wa Muslim Brotherhood mwezi Julai mwaka jana.
- Bbc
Post a Comment