
Polisi wakikabiliana na waandamanaji nchini Misri
Maafisa wa usalama nchini Misri
wanasema afisa wa ngazi ya juu wa polisi nchini Misri ameuawa katika
shambulio la bomu katika mji mkuu Cairo.
Polisi huyo Brigedia Generali Ahmed Zaki aliuawa
katika kitongoji cha Magharibi mwa mji huo baada ya bomu lililokuwa
limetegwa chini ya gari lake kulipuka.
Shambulio hilo ni la hivi karibuni
katika mfululizo wa mashambulizi dhidi ya vikosi vya usalama tangu
kung'olewa madarakani kwa aliyekuwa Rais Mohamed Morsi Mwezi Julai mwaka
jana
Mjini Alexandria,afisaa mwingine mmoja aliuawa wakati wa shambulizi dhidi ya kile maafisa wanasema ni maficho ya wanamgambo.
Wapiganaji wa kiisilamu wameongeza kasi ya
mashambulizi dhidi ya maafisa wa usalama na kuwaua mamia tangu jehi
kumwondoa mammalakni Morsi.
Mnamo siku ya Jumapili, mtu aliyekuwa amejihami
kwa bunduki alimpiga risasi na kumuua afisaa mmoja wa polisi aliyekuwa
anashika doria.
Shambulizi hilo lilitokea siku moja baada ya polisi mwingine kuuawa mjini Cairo na kundi la wapiganaji wajulikanao kama Ajnad.
Kundi hilo linasema linashambulia polisi kwa
sababu ya msako unaofanywa dhidi ya kundi la Muslim Brotherhood. Zaidi
ya watu 1,300 wameuawa na wengine
16,000 kuzuiliwa.
Ghasia hizi huenda zikatishia usalama wakati wa
uchaguzi mkuu utakaofanyika mwezi Mei, ambapo aliyekuwa mkuu wa majeshi
Abdul Fattah al-Sisi anatarajiwa kushinda
- bbc
Post a Comment