Asia Idarous: Muziki wa mwambao asilia una mguso wake

Na Andrew Chale
MWANAMITINDO mkongwe na mdau wa muziki wa mwambao asilia, Asia Idarous Khamsin, amesema muziki huo una mguso wake hivyo jamii inatakiwa kuupokea na kuuenzi.
Asia ambaye pia ni Mkurugenzi wa Fabak Fashions, alisema hayo usiku wa April 19, wakati wa onesho maalumu la Usiku wa Mwambao Asilia, ambalo pia lilihudhuriwa na Katibu Mkuu wa zamani wa Umoja wa Nchi Huru za Afrika (OAU, sasa AU), Dk. Salim Ahmed Salim, aliyekuwa mgeni rasmi akiungana na wadau wengine katika kuenzi muziki huo ndani ya ukumbi wa Travertine, Magomeni jijini Dar es Salaam.
Asia alisema katika kuenzi muziki huo ni pamoja na kuwakumbuka wanamuziki wakongwe walioufikisha hapo ulipo.
“Baadhi ya nyimbo za mwambao asilia unapozisikiliza zinagusa moja kwa moja, na ujumbe wake hufika kwa haraka,” alisema Asia.
Katika onesho hilo, Asia alidhihirisha umahiri wake na kuimba kibao cha ‘Raha ya Moyo Wangu’.
Bendi za Dar Modern Taarab na Nadd Ikhwan (Malindi), zilikonga nyoyo wadau wa miondoko hiyo waliofurika ndani ya ukumbi huo huku wakipata pia wasaha wa kupita kwenye zuria jekundu na kupiga picha za ukumbusho, ambapo awali kwenye miondoko ya taarab hapa nchini haikuwa na utamaduni huo wa red carpert.
Onesho hilo lilidhaminiwa na Times FM, Fabak Fashions na www.nakshi255.com  na wengine wengi wakiwemo mashughuli blog, Michuzi blog, Vijimambo blog simu tv na wengine wengi.








Post a Comment

Previous Post Next Post