Iliwahi
kutokea Tabata Dar es salaam akakamatwa askari feki wa usalama
barabarani ambae ni mzee aelikua anavalia sare na madereva walikua
wanajua kweli huyu ni askari na faini na rushwa akawa anazilamba kama
kawaida.Stori nyingine kwenye headlines sasa hivi ni za Mwanajeshi feki
nchini Kenya ambapo kituo cha TV cha K24 ndio kimeripoti hii stori kwa
kusema jamaa alishtukiwa na Mwanajeshi halisi wa nchi hiyo.
Huyu
jamaa mwenye umri wa miaka 23 alikamatwa wakati akiwa anasafiri, anaitwa
Robert Mutuku na anakiri alipata hizi jezi za jeshi kutoka kwa rafiki
yake ambae alikua anamtafutia kibarua jeshini.Akiwa tayari anashikiliwa
na polisi, Mutuku ambae pia alikua na kitambulisho feki cha jeshi
amekaririwa akisema ‘ni kazi nilikua naitaka ndio maana niliomba hizi
nguo kwa sababu naipenda hii kazi’
Post a Comment