Ni siku chache tu zimepita toka Paul Okoye wa kundi la P-Square
afanye harusi ya kimila na mke wake Anita Isama huko Nigeria, lakini
baada ya wote wawili (Peter & Paul) kukamilisha majukumu ya ndoa
zao, kuna habari ambazo zimesambaa wiki hii kuwa umeibuka ugomvi baina
ya mapacha hao wa kundi la P-Square ambao inasemekana sasa hawaelewani
vizuri.
Mtandao wa Naija Gists umeripoti kuwa kwa mujibu wa chanzo, inadaiwa
kuwa kumekuwa na kutoelewana baina ya kaka mkubwa wa mapacha hao Jude
Okoye na mke wa mdogo wake Peter Okoye aitwaye Lola Omotayo, kitu
kilichopelekea Jude kutohudhuria harusi yao mwaka jana.
Kama unakumbuka Jude hakuhudhuria harusi ya Peter na Lola mwaka jana,
lakini alihudhuria ya Paul na Anita mwaka huu kitu kinachowafanya watu
waamini kuwa kuna tatizo kubwa baina yao.
Chanzo hicho kimesema inadaiwa kuwa ugomvi huo unaomhusu Lola
umesababisha Peter na Paul kugombana wakati wako kwenye rehearsle
Jumatano wiki hii, mpaka walipoachanishwa na dancers wao.
Peter na Paul na wake zao Lola na Anita
Kaka mkubwa wa P-Square Jude alitweet kitu ambacho kinaaminika kuwa kinahusiana na ugomvi wao.
“After over 10 years of hard work, it’s over. (I) Am done.”
ikiaminika kuwa alimaanisha amejiondoa kuli-manage kundi hilo japo kuwa
yeye mwenyewe hakufafanua alichomaanisha katika maneno hayo machache.
After over 10yrs of hard work, it's over. Am done.
— IG: @Judeengees (@judeengees) April 18, 2014
Jude ndiye amekuwa akiwa-manage kwa miaka yote na kuproduce hits zao
paomoja na kudirect idadi kubwa ya video zao zilizofanya vizuri.
Lakini kuna baadhi ya watu nchini Nigeria wamedai kubwa kuna
uwezekano kuwa ugomvi ‘hewa’ unaoendelea na kuripotiwa katika vyombo vya
habari ukawa ni ‘hype’ ya kuandaa ‘kiki’ ya album yao mpya.
Source: Naija Gists
Post a Comment