BREAKING NEWS;- Radio hii 93.7 YAFUNGIWA na serikali

.
dj-choka-top-web-banner
Baada ya kuwa gumzo kwa takriban wiki tatu kituo cha Radio ambacho kilikuwa kitumie masafa ya 93.7 FM DSM ambacho kililikuwa kwenye hatua za mwisho mwisho kabisa za maandalizi ya kuanza kurusha matangazo yake mwishoni mwa mwezi huu inasemekana kimefungiwa
Kwa mujibu wa nyepesi nyepesi kutoka kwa mapaparazi wetu waliokuwa wakifuatilia habari juu ya kituo hicho kutoka kwa vyanzo vyetu makini vilivyo karibu na wanaojiita wadau wa Radio hiyo, kituo hicho kimepigwa marufuku baada ya kukiuka miiiko na maadili ya tasnia ya habari nchini.
Chanzo chetu cha uhakika kimetuambia kwamba Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imesitsha usajili wa Redio hiyo baada ya wamiliki wake, kuanza kuitangaza kwenye mitandao ya kijamii na kuanza kupiga muziki holela kabla hata ya tarehe rasmi ya kuanza kurusha matangazo.
Radio hiyo ambayo masafa yake ya 93.7 FM DSM yalianza kuwa gumzo jijini Dar-Es-Salaam kabla hata ya kuanza rasmi inasemekana ilikuwa tayari imeshakamilisha kazi ya kupitia usaili wa watangazaji na ma dj watarajiwa, ambapo ndani yake kulikuwa na mseto wa nguvu.
Chanzo chetu kiliendelea kutuhabarisha kuwa katika kutaka kunogesha uanzishaji wa Radio hiyo, katikati ya wiki iliyopita wamiliki walikuwa tayari wamefanya booking ya wasanii Snoop Doggy Dog, Lil Wayne na Nicky Minaj kwa ajili ya kuja kuzindua rasmi Radio, huku DJ maarufu jijini Atlanta DJ Khaleed pamoja na mchezaji maaarufu wa Italia anayechezea AC Millan Mario Baloteli alikuwa amekubali kuwa Guest Star wa kipindi cha michezo baada ya kuisha kwa mashindano ya ligi Italia.
Aidha chanzo chetu kilisema pamoja na kufungiwa uongozi unajitahidi kupambana ili kuondolewa adhabu hiyo ili irudi hewani. Kama ilivyo ada yetu tutaendelea kufuatilia kwa karibu na kukuhabarisha.

http://djchokamusic.

Post a Comment

Previous Post Next Post