
Tangu sakata hilo la Dayna na Diamond kuisha, mwandada huyu amekua hasikiki sana katika masikio ya watu. Kwani hajatoa wimbo mpya kwa mda mrefu sasa. Dayna akihojiwa na tovuti ya BaabKubwa kuhusu ukimya wake katika game alisema “Siyo kama nipo kimya nimeishiwa hapana ila nilikuwa nina majukumu ya kifamilia kidogo, pamoja na kuendelea kusoma game coz kila siku muziki unakuwa na mashabiki wanahitaji vitu vipya kwa hiyo kama msanii hautakiwi kukurupuka katika kutoa wimbo. Nimefanya nyimbo nyingi ila kwa sasa naangalia ipi ianze so mashabiki wangu wakae tayari any days naachia jiwe jipya na siwezi kuwaangusha.”
Post a Comment