![]() |
Girlfriend wa Hemedy |
Hemedy PHD amesema girlfriend wake aliyemtambulisha wazi ndiye aliyemvutia kuandika wimbo wake ujao uitwao ‘On My Wedding Day’.
Amesema amekuwa akifuatilia maisha ya mastaa wa nje na kugundua kuwa
wengi wamekuwa wakiyaweka wazi mahusiano yao tofauti na wasanii wa
Tanzania na ndio maana naye ameamua kumweka wazi na kuwa huru.
“Kwasababu ni demu ambaye nina uhakika naye, demu ambaye moyo wangu
naona kabisa umependa nikapata mpaka mawazo kwamba one day nahisi huyu
ndiye atakayekuja kuwa one and only wa kumuoa ndio hiyo idea ya kuandika
hiyo ngoma ikaja,” amesema.
Hemedy ameongeza kuwa ameandika wimbo huo kwakuwa anaamini kuwa
harusi ni sherehe zilizopo katika maisha yote ya binadamu na hivyo kama
ukipendwa unaweza kumletea neema. Amesema pia kuwa mashabiki wake
wategemee video ya tofauti sana ya wimbo huo na hadi sasa amekuwa
akiumiza kichwa namna ya kuifanya isiwe ya kawaida.

Post a Comment