
Lema aliyasema hayo jana Jijini hapa wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari Jijini hapa
Alisema
aliomba kibali cha kufanya mikutano na wananchi wa jimbo lake mwezi huu
lakini cha ajabu alijibiwa na polisi kuwa hataweza kuruhusiwa kufanya
mikutano kutokana na hali za usalama.
Alisema awali alipokea barua
kutoka polisi ya kuzuiwa kufanya mkutano wake leo ,na kusisitiza kuwa
yeye ni mbunge anahaki ya kufanya mikutano na wananchi wake ili kujua
kero mbalimbali wanazokutana nazo nay eye kuzishughulikia.
"Wananchi
wangu wamevunjiwa nyumba, madiwani wamepigwa na mgambo, mgambo hao hao
wanawazuia wananchi wasifanye biashara bado wanakero nyingi sasa naomba
kibali polisi wanakataa yani mikutano yangu ndio inasababu za kiusalama
lakini kwenye kumbi za starehe na maeneo mbalimbali wanaruhusiwa kufanya
mambo yao."
"Polisi nataka wajue ya kuwa mimi ni Mbunge wa
kuchaguliwa na wananchi na wananchi wanahitaji kuongea na Mbunge wao
halafu wananizuia lakini mimi nasema watake wasitake leo ntafanya
mkutano na kama ni kesi wanibambikie maana kama mbunge ninahaki ya
kuongea na wananchi wangu ,sasa naomba kibali wanaweka vizuizi hivyo leo
nitaongea na wananchi wangu eneo la Kilombero viwanja vya Samunge.
Akizungumzia
kuhusu bunge la Katiba ,Lema alisema Bunge hilo badala ya kujadili
suala la katiba limekuwa ni bunge la matusi na dhihaka ambalo haliwezi
kuendelea kutokana na wajumbe kumshambulia mtu mmoja mmoja badala ya
maslahi ya nchi.
Kuhusu kuzuiwa mikutano yake na Jeshi la Polisi
alisema aliandika barua kuomba ulinzi Aprili 17 mwaka huu akiomba
kufanya mikutano kwenye kata tatu za Manispaa ya Arusha, lakini polisi
walimjibu wakisema CCM walishaomba nao Aprili 19 mwaka huu, kufanya
mikutano kwenye maeneo hayo aliyoomba yeye kufanya mkutano wake.
"Nashangaa
polisi wanazuia mikutano yangu lakini wanaruhusu mikutano ya Injili na
starehe katika kumbi mbalimbali, ila mimi kuongea na wananchi wangu
wanazui hii haikubaliki na nitafanya," alisema.
Alisema kutokana na
kukaa nje ya Jimbo lake kwa muda mrefu na anatarajia kuondoka tena kwa
zaidi ya miezi miwili kwa ajili ya bunge la bajeti, alisema ndio sababu
kubwa inayomsukuma kuongea na wananchi wake waliokumbw ana mambo mengi
ikiwemo bomoabomoa.
Pia sababu nyingine anayotaka kuongea na wananchi wake kutokana na mchakato wa katiba mpya ambao lazima auzunguzie.
Hata
hivyo alimpongeza Mkuu wa Mkoa Arusha, Magesa Mulongo kuhutubia
wananchi kupitia Redio '5' kuwa hakuna sababu z amsingi za kuzuia
mikutano hiyo jambo ambalo alisema ni la kweli.
Naye Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Saba alipoulizwa na waandishi wa habari
juu ya kuzuia mkutano wake , alisema wameruhusu baada ya kujiridhisha
na hali ya usalama.
"Huko nyuma tulizuia kutokana na hali ya usalama
ila sasa tumejiridhisha nimetoka kuongea na OCD kuwa awaruhusu kufanya
mkutano na utafanyika leo," alisema Sabas.
Wakati huo huo, Lema
alisema bunge la Katiba limekuwa ni bunge la kujadili mtu mmoja mmoja
badala ya kujadili suala la katiba na kushangazwa na wabunge baadhi
kuchangia hoja za matusi matusi na dhihaka .
Post a Comment