Mwenyekiti
 wa Jukwaa la Katiba, Deus Kibamba akizungumza katika mkutano wa 
waandishi wa habari uliofanyika ofisi za Jukwaa la Katiba jijini Dar es 
Salaam katika kutoa tamko rasmi za tathimini ya Jukwaa la Katiba 
Tanzania kuhusu Katiba Mpya, Tulipotoka, Tulipo na Tuendako. Pembeni ni 
Msimamizi wa Mradi wa taasisi isiyo ya kiserikali ya (NGO Network for 
Dodoma) Bw. Edward Mbogo (kushoto) na Mjumbe wa Jukwaa la Katiba toka 
Pemba Bw. Omari Omari.


Waandishi wa Habari wakifuatilia.
---
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam.
Jukwaa
 la Katiba Tanzania (JUKATA) limejitolea kuratibu maridhiano  miongoni 
mwa makundi ya kisiasa  asasi za kiraia, asasi za wananchi na taasisi 
zote za muhimu zilizoguswa na migogoro inayoendelea katika Bunge maalum 
la katiba Tanzania.
Akizungumza
 na waandishi wa habari katika ofisi za Jukwaa la Katiba jijini Dar es 
Salam, Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba Bw. Deus Kibamba  juu ya tathimini
 walizozifanya katika bunge hilo wameamua kujitolea kufanya maridhiano 
hayo kwa kuwashirikisha viongozi maarufu Afrika Mashariki  akiwemo 
mheshimiwa jaji mkuu mstaafu wa Tanzania, Barnabas Samatta ambaye 
atakuwa mkuu wa jopo hilo la usuluhisho  na ndugu  Patrice Lumumba kutoka nchini Kenya ambaye atakuwa msaidizi.
Aidha 
jukwaa hilo limeonyesha masikitiko yake kwa kile alichookiita ni 
uvunjifu wa kanuni mara baada ya wabunge zaidi ya mia mbili kutoka nje 
lakini wabunge waliobakia kuendelea kurekebisha kanuni za bunge hilo 
jambo ambalo wamesema kuwa haikustaili kwani wana uwezo wa kujitungia 
sheria.
Kibamba
 amesema kuwa kutokana na mwenendo wa bunge hilo hadi hapa lilipofikia 
wabunge hao hawana nia ya dhati ya kulipatia taifa katiba mpya huku 
akitolea mfano kuwa katiba mpya ilipangwa kuwekwa  saini na Rais siku ya
 tarehe 26 mwezi huu  yani leo lakini hadi sasa hata majadiliano ya sura
 mbili hayajamalizika, na kuwahakikishia watanzania kuwa hakuna katiba 
mpya itakayopatikana kwa mwaka huu.
Hata 
hivyo mwenyekiti huyo amewataka wajumbe wote na asasi zote zilizopo nje 
ya muendelezo wa bunge hilo maalumu la katiba kuwa tayari kwa maridhiano
 kwa mtu au taasisi yoyote atakayekuwa tayari kutatua migogoro yao ili 
kuwezesha upatikanaji wa katiba kwa taifa letu.

Post a Comment