Muonekano wa Kiwanda cha Sukari Mahonda kilivyo hivi sasa.
Mshauri muelekezi wa Kiwanda cha Sukari
Mahonda Dk. Hamza Hussein Sabri (alie simama) akitoa maelezo na
changamoto wanazozipata Kiwandani hapo, kwa Kamati ya Fedha, Biashara na
Kilimo ya Baraza la wawakilishi walipoenda kutembelea Kiwanda hapo.
Makamo Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha,
Biashara na Kilimo ya Baraza la wawakilishi Hija Hassan Hija akizunguza
na uongozi wa Kiwanda cha Sukari na viongozi wa Wizara ya Biashara,
Viwanda na Masoko katika kuangalia hatua ya uzalishaji Sukari Kiwandani
hapo na changamoto wanazokabiliana nazo.
Afisa utumishi wa Kiwanda hicho Bw. Bashir Mohammed akionyesha kiroba cha kilo 50 za Sukari.
Mkurugenzi wa maendeleo ya viwanda
Wizara ya Biashara, Viwanda na Masoko Zanzibar Bw. Saleh Suleiman Hamad
akiwaonyesha wajumbe wa Baraza la wawakilishi Sukari iliozalishwa
kiwandani hapo ambayo bado haijaingia sokoni hadi sasa.
(Picha zote na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar).
Post a Comment