Kocha wa timu wa taifa ya Uholanzi Louis van Gaal amekubali kuwa
kocha ya kudumu wa klabu ya Manchester United kwa mkataba mfupi
usiozidi miaka mitatu.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mtandao wa Goal zinasema Van
Gaal amekubali kukinoa kikosi cha Manchester United na kwa mkataba mfupi
usiozidi miaka mitatu na atakichukua kikosi hicho baada ya kumalizika
kwa Kombe la Dunia itanayotajia kuanza mwezi ujao huko Brazil.
Taarifa hiyo imeendelea kusema kuwa Makamu mwenyekiti wa Manchester
United Ed Woodward pamoja na moja ya wamiliki wa klabu hiyo wamekuwa
kwenye mazungumzo na kocha huyo.
Pia taarifa hiyo imesema United ajaweza kuweka wazi uvumi huo na
kudai kuwa United bado wapo kwenye makubaliano toka pande zote mbili.
Source:Goal
Post a Comment