KOCHA
wa Simba SC, Zdravko Logarusic aondoka leo kwenda mapumzikoni nyumbani
kwao Croatia, baada ya kukubaliana na uongozi wa klabu hiyo kuendelea
kuifundisha timu hiyo.
Logarusic alikuwa na kikao leo na Mwenyekiti wa
Kamati ya Usajili ya timu hiyo, Zacharia Hans Poppe na amepewa stahiki
zake zote kuelekea likizo hadi Juni.
“Logarusic
ataendelea na kazi Simba SC, ni mwalimu ambaye wadau wote wa timu yetu
wamemkubali na wameona bora wampe muda zaidi kuona na msimu ujao atavuna
nini,”kimesema chanzo kutoka Simba SC.

REKODI YA LOGARUSIC SIMBA SC;
Simba SC 3-1 KMKM (Kirafiki)
Simba SC 3-1 Yanga SC (Mtani Jembe)
Simba SC 1-0 KMKM (Kombe la Mapinduzi)
Simba SC 2-0 Chuoni (Robo Fainali Mapinduzi)
Simba SC 2-0 URA (Nusu Fainali Mapinduzi)
Simba SC 0-1 KCC (Fainali Kombe la Mapinduzi)
Simba SC 0-1 Mtibwa Sugar (Kirafiki)
Simba SC 1-0 Rhino Rangers (Ligi Kuu Bara)
Simba SC 4-0 JKT Oljoro (Ligi Kuu Bara)
Simba SC 1-1 Mtibwa Sugar (Ligi Kuu Bara)
Simba SC 0-1 Mgambo JKT (Ligi Kuu Bara)
Simba SC 1-1 Mbeya City (Ligi Kuu Bara)
Simba SC 2-3 JKT Ruvu (Ligi Kuu Bara)
Simba 3-2 Ruvu Shooting (Ligi Kuu Bara)
Simba SC 0-0 Prisons (Ligi Kuu Bara)
Simba SC 0-1 Coastal Union (Ligi Kuu)
Simba SC 1-2 Azam FC (Ligi Kuu)
Simba SC 1-1 Kagera Sugar (Ligi Kuu)
Simba SC 0-1 Ashanti United (Ligi Kuu)
Simba SC 1-1 Yanga SC (Ligi Kuu)
Kwa upande mwingine, kipa Mghana Yanga Berko yeye hataongezewa Mkataba baada ya kumaliza Mkataba wake wa wa miezi sita.
Simba SC inaachana na Berko ili kusajili kipa mzalendo na kutoa nafasi za wachezaji wa ndani wa kigeni.
Mabeki
Mkenya Donald Mosoti na Mganda Joseph Owino wote wataongezewa mikataba
na mshambuliaji Mrundi Amisi Tambwe, wakati mwenzake Kaze Gilbert
ameonyeshwa mlango wa kutokea.
![]() |
| Nje; Yaw Berko amefungwa mabao sita katika mechi tano na kwa sababu hiyo haongezwi mkataba |
REKODI YA YAW BERKO SIMBA SC
Simba SC 3-1 KMKM (Kirafiki, alifungwa moja Dar)
Simba SC 1-0 KMKM (Kombe la Mapinduzi, hakufungwa)
Simba SC 0-1 Mtibwa Sugar (Kirafiki, alifungwa moja)
Simba SC 1-1 Mbeya City (Ligi Kuu Bara, alifungwa moja)
Simba SC 2-3 JKT Ruvu (Ligi Kuu Bara, alifungwa tatu)
Orodha
ya wachezaji wa kuongeza kikosini kwa ajili ya msimu ujao tayari
Logarusic amekwishaiwasilisha kwa Hans Poppe ambaye anaanza kuifanyia
kazi kuanzia kesho.
Logarusic
aliyejiunga na Simba SC Desemba mwaka jana, amekwishaiongoza timu hiyo
katika mechi 20 za mashindano yote, akiiwezesha kushinda mechi nane,
sare tane na kufungwa saba, wakati Berko ameidakia Simba SC mechi tano
na kufungwa jumla ya mabao sita.
Credit.Bin zubeiry

Post a Comment