Mwigizaji wa Kenya Lupita Nyong’o ameweka rekodi nyingine kwa
kufikisha followers milioni 1 katika mtandao wa Instagram ambao mpaka
leo tayari ana 1,007,570.
Kwa mujibu wa Nairobi Wire, Lupita ndio amekuwa Mkenya wa kwanza
kufikisha followers wengi Instagram, huku upande wa Facebook mchekeshaji
wa Kenya Daniel Churchill ndiye Mkenya wa kwanza aliyefikisha likes
Millioni moja wiki iliyopita.
Mastaa wengine wa Kenya ambao wameachwa mbali na Lupita kwa kuwa na
followers wachache Instagram ni pamoja na Prezzo mwenye 28,000+
Victoria Kimani ambaye ana 17,000+ na video vixen Vera Sidika ambaye ana
15,000+.
Kwa upande wa Tanzania Diamond Platnumz na Wema Sepetu ndio mastaa
wenye followers wengi zaidi, Diamond akiwa na 106,000+ na mpenzi wake
Wema akiwa na 95,000+.

Post a Comment