Hali hiyo
ilijitokeza juzi na kusababisha baadhi ya ndugu wa mahabusi hao
waliokuwa mahakamani hapo kusikiliza kesi, kukimbia kuepuka kushuhudia
ndugu zao wakivua nguo.
Mahabusi hao, wengi wakiwa ni wenye kesi za dawa za kulevya
, wizi wa kutumia silaha na mauaji, walidai wamekaa mahabusu zaidi ya
miaka miwili bila kusomewa maelezo ya awali katika kesi zao huku
wakiendelea kuteseka gerezani.
Awali kabla ya kuvua nguo,
walipofikishwa juzi mahakamani saa 3.15 asubuhi wakiwa ndani ya basi la
Magereza lenye namba za usajili MT 0041, waligoma kushuka wakitaka
kupewa maelezo ya kujitosheleza kutoka kwa Msajili wa Mahakama Kuu
Kanda ya Arusha juu ya malalamiko yao.
Askari magereza waliomba
kuongezewa idadi na ndipo askari zaidi ya 15 waliletwa wakiwa kwenye
gari aina ya Land Cruiser lenye namba za usajili MT 0075.
Baada ya
mahabusi kuona ulinzi umeimarishwa huku basi lao likiwa limezingirwa na
askari Magereza wenye silaha za moto, waliamua kuvua nguo zote huku
wakiimba na wengine wakipiga kelele za kutaka kufahamu hatma ya kesi
zao.
Akizungumzia suala hilo jana, Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya
Arusha, Willberd Mashauri alisema hakuwepo mahakamani. Alisema alikuwa
katika vikao vya Mahakama Kanda ya Arusha.
Hata hivyo alikiri
malalamiko ya mahabusi hao kuwepo na kwamba yanafanyiwa kazi. Agosti
mwaka jana, mahabusi hao pia waligoma kushuka kwenye basi lao
wakishinikiza kesi zao zianze kusikilizwa.
Post a Comment