![]() |
| Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka akizungumza wakati wa uzinduzi wa mashindano hayo. Wa pili kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Chiku Matesa. |
MASHINDANO
ya Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii inayowahusisha waandishi wa
habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari (NSSF Media Cup) yameanza
kutimua vumbi katika uwanja wa TCC, Chang'ombe jijini Dar es Salaam.
Akifungua
mashindano hayo, Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudencia Kabaka, amewataka
wanahabari nchini kuhakikisha wanajiunga na Shirika la Taifa la Hifadhi
ya Jamii (NSSF), ili kujihakikishia maisha ya amani na utulivu baada ya
kustaafu.
Alisema
kuwa, wanahabari wanapaswa kwenda mbali zaidi katika kulitumia shirika
hilo, ili kunufaika na mafao mbalimbali yanayotolewa kwa wanachama.
Katika
ufunguzi huo, timu ya soka ya New Habari (2006) Ltd iliumana na Habari
Zanzibar katika Soka, ambako hadi filimbi ya mwisho Habari Zanzibar
iliibuka kidedea kwa magoli 4-1, magoli ya Zanzibar yaliwekwa wavuni na
Amoor Suleiman aliyeweka wavuni goli moja na Yusuph Juma magoli matatu
huku goli la New Habari likiwekwa wavuni na Florian Mwasinde.
Kwa
upande wa netiboli, timu ya Jambo Leo iliichapa timu ya Wizara ya
Habari Bara kwa jumla ya magoli 59-8, katika pambano la upande mmoja
lilipoigwa kwenye viwanja hivyo.
Katika
mechi ya pili ya netiboli, Azam Media iliumana na Tanzania Standards
Newspaper (TSN), ambako Azam waliibuka washindi kwa magoli 18-13.
Kabaka
aliwataka washiriki wa mashindano hayo ya 11 yanayoshirikisha
wafanyakazi wa vyombo vya habari kuonesha ushindani, ufundi na nidhamu
ili kuongeza hamasa ya michuani hiyo.
Alivitaka
vyombo vya habari kuepuka kuingiza wachezaji wasio wanahabari
(mamluki), kudumisha lengo la umoja na ushirikiano baina ya shirika hilo
kongwe na vyombo vya habari, ikiwamo kuwapa mazoezi wafanyakazi wa
vyombo hivyo.
Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia
Kabaka (wa pili kulia), akipata maelezo kutoka kwa Ofisa Uhusiano wa
Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Carolyne Newa wakati
alipotemberlea banda la NSSF wakati wa uzinduzi wa mashindano ya NSSF
Media Cup 2014 kwenye uwanja wa TCC Chang’ombe jijini Dar es Salaam.

Waziri
wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka akisalimiana na mshambuliaji wa timu
ya New Habari 2006, Joh Dande wakati wa uzinduzi wa michuano ya NSSF
Media Cup 2014 kwenye uwanja wa TCC Chang'ombe Dar es Salaam.
Mchezaji
wa New Habari, Jonathan Tito, akimiliki mpira huku akizongwa na
mshambuliaji wa timu ya Habari Zanzibar, Hamza Hamza katika mchezo wa
ufunguzi wa michuano ya NSSF Media Cup uliofanyika kwenye Uwanja wa TCC,
Chang’ombe jijini Dar es Salaam jana. Habari Zanzibar ilishinda 4-1.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Chiku Matesa (kulia), akibadilishana mawazo na Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka wakati wa uzinduzi wa michuano hiyo.

Mchezaji
wa timu ya netiboli ya Jambo Leo (kushoto), akimiliki mpira wakati timu
hiyo ilipopambana Habari-Maelezo. Jambo leo ilishinda ilishinda 60-8
Mchezaji
wa timu ya netiboli ya Jambo Leo (kushoto), akimiliki mpira wakati timu
hiyo ilipopambana Habari-Maelezo. Jambo leo ilishinda ilishinda 60-8

Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka akizundua michuano ya netiboli ya NSSF Media Cup.

Kikosi cha Jambo Leo.





Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Chiku Matesa akisalimiana na wachezaji wa timu
ya Azam Media wakati wa ufunguzi wa michuano ya NSSF Media Cup 2014.
Wasanii wa kikundi cha Dar Greater wakitumbuiza wakati wa hafla hiyo.


Post a Comment