
Kampuni
ya Vodacom Tanzania kwa kushirikiana Taasisi ya Malaria No More na
THT(Tanzania house of talent) leo wameitangaza rasmi nambari maalum
ambayo wateja wanaotumia huduma za Vodacom wanaweza kuitumia kupata
taarifa zinazohusiana na ugonjwa wa malaria.
Ili
mteja kuweza kupata taarifa hizo zinazohusisha jinsi ya kujikinga, tiba
na masuala mengine mbalimbali ya Malaria anachopaswa mteja kufanya ni
kujiunga kwa kutuma neno "Malaria" au "Mzinduka" kwenda nambari 15760
bila malipo.
Ujio
wa huduma hii ni sehemu ya kampeni kabambe ya Mzinduka inayolenga
kuongeza kasi katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa malaria hapa nchini
ambayo Vodacom Foundation ni mshirika wake.
Nambari
hiyo imetangazwa jijini dar es salaam kwenye uwanja wa taifa muda mfupi
kabla ya kuanza kwa mechi kati ya Simba na Yanga kwa lengo la
kuwashirikisha washabiki wa soka nchini kuunga mkono kampeni hiyo.
"Ni
imani yetu kuwa kupitia huduma hii wananchi watakuwa na fursa rahisi na
nyepesi ya kujua mambo mbalimbali yanayohusu malaria na ni kwa njia hiyo
tunaweza kuishinda vita dhidi ya ugonjwa huo hatari unaoongoza kwa
kusababisha vifo ikiwemo wanaawake wajawazito na watoto wenye umri chini
ya miaka mitano"alisema Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim
Amesema
kampuni ya Vodacom kupitia mfuko wake wa kusaidia jamii wa Vodacom
Foundation imeona umuhimu wa kuunga mkono kampeni hiyo kutokana na
ukweli kwamba ugonjwa wa malaria ni tishio na kwamba maisha ya watu
lazima yalindwe.
"Kupitia
Vodacom Foundation, Tumefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuunganisha watu na
kuyabadili maisha yao kupitia teknolojia ya simu za mkononi na sasa
tunataka tuitumie teknolojia hiyo ya simu za mkononi kuokoa maisha yao,
hii ni njia rahisi na isiyo na gharama kwa mteja wetu."Aliongeza Mwalim
Amesema
wameutumia mchezo wa Simba na Yanga kutangaza nambari hiyo ikitambua
ukubwa wa mtandao wa washabiki wa mpira wa miguu nchini ambao ukitumika
vema ni wazi utatoa mchango mkubwa katika kuipatia kampeni hiyo ufanisi.
"Tunataka
ujumbe huu ufike kwa kila mtanzania ili kwa pamoja tuweze kuhakikisha
kila mmoja wetu ana taarifa sahihi za malaria na hivyo kulinda maisha
yake na ya wanaomzunguka,kupitia michezo hususan soka hilo linawezekana
kwa wepesi na haraka zaidi"
Kwa
muda wa miaka 10 sasa iliyopita Tanzania imekuwa kati ya nchi
zilizokuwa kwenye mstari mbele kupigana na ugonjwa huu wa malaria na
vimepungua kwa asilimia 50.
Kwa
upande wake mwakilishi wa Taasisi ya Malaria No More Lilian Madeje
ametoa rai kwa watanzania kuitumia huduma hiyo ili kupunguza pengo la
upatiakanaji wa taarifa sahihi zinazohusu Malaria
"Pamoja
na kuwepo na changamoto nyengine kadhaa katika vita dhidi ya malaria
bado suala la wananchi kuwa na taarifa sahihi za malaria ni jambo la
muhimu ili kumuwezesha kila mmoja kutambua namna ya kujikinga, kugundua
viashiria ama dalili za ugonjwa wa malaria na namna ya kupata tiba bora
na iliyo sahihi."
Amesema
mara mteja anapojiunga atakuwa akipokea taarifa mbalimbali bila ya
gharama yoyote na mutoa rai kwa kila mmoja kuwa balozi kwa mwenzake
katika kuhamamisha matumizi ya huduma hiyo.
Huduma hiyo ni sehemu ya kampeni ya Mzinduka iliyozinduliwa na Makamunwa rais Dk Mohamed Gharib Bilala Disemba mwaka jana.
Chini
ya kampeni hiyo, njia mbalimbali zenye mvuto kwa makundi kadhaa hususan
vijana zinatumika katika kueneza ujumbe wa malaria na kuishajihisha
jamii kuunga mkono vita dhidi ya ugonjwa wa malaria nchini.
Post a Comment