
Lionel Messi akishangilia baada ya bao lake la ushindi aliloifungia Barcelona usiku wa jana
NYOTA Lionel Messi amehitimisha dakika
348 za kucheza bila kufunga bao, akiiwezesha Barcelona kushinda mabao
2-1 dhidi ya Athletic Bilbao katika La Liga.
Muargentina huyo alifunga kwa mpira wa
adhabu dakika mbili baada ya Pedro had kusawazisha dhidi ya Athletic
Bilbao Uwanja wa Nou Camp.
Messi aliyecheza mechi tatu bila
kufunga, usiku wa jana alifunga bao lake dakika ya 74 wakati Pedro
alifunga dakika ya 72 baada ya wageni kutangulia kupata bao dakika ya 50
kupitia kwa Aduriz.
Barcelona imefikisha pointi 81 baada
ya kucheza mechi 34 na inarudi nafasi ya pili, nyuma ya Atletico Madrid
yenye pointi 85 za mechi 34 pia, wakati Real Madrid ina pointi 79 za
mechi 33 na Jumamosi itacheza na Osasuna
Post a Comment