
Naibu
Waziri wa Fedha na Mbunge wa jimbo la Iramba magharibi, Mh.
Mwigulu
Nchemba akihutubia wapiga kura wake na wananchi wa kata ya Mtoa tarafa
ya Shelui ambapo pamoja na mambo mengine, alihimiza ujenzi wa zahanati
kwa kila kijiji.

Naibu
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk.Kebwe Stephen Kebwe (MB)
akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha
Mgongo tarafa ya Shelui jimbo la Iramba magharibi ambapo amewataka
Wakurugenzi wa halmashauri za majiji, manispaa na wilaya kuhakikisha
magari ya kubebea wagonjwa hayatumiki kusafirisha bidhaa yoyote ikiwemo
mkaa.

Baadhi
ya wakazi wa kata ya Kyengenge jimbo la Iramba magharibi, wakimsikiliza
Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk.Kebwe Stephen Kebwe (hayupo
kwenye picha) ambaye aliwataka waganga wakuu wa halmashauri za majiji,
manispaa na wilaya, kusimamia kikamilifu matumizi ya dawa na vitendea
kazi.

Ambulince
T.821 CUV iliyotolewa msaada na mbunge wa jimbo la Iramba magharibi,
Mh. Mwigullu Nchemba kwa wakazi wa tarafa ya Shelui.Ambulance hiyo
imemgharimu Mwingullu zaidi ya shilingi 50 milioni.

Mbunge
wa jimbo la Iramba magharibi, Mh. Mwigullu Nchemba akisalimiana na timu
ya soka ya kijiji cha Kyengenge.(Picha zote na Nathaniel Limu).
Na Nathaniel Limu
SERIKALI
imewaonya wakurugenzi wa halmashauri za majiji, manispaa na wilaya
nchini, kuhakikisha wanasimamia kikamilifu matumizi sahihi ya magari ya
kubebea wagonjwa (Ambulance), vinginevyo watachukuliwa hatua kali za
kisheria.
Onyo
hilo limetolewa na Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Kebwe
Stephen Kebwe (Mb), wakati akizungumza kwenye hafla iliyofana ya
kukabidhi msaada wa gari la kubebea wagonjwa (Ambulance), lililotolewa
na mbunge wa jimbo la Iramba magharibi, Mwigulu Nchemba kwa wakazi wa
tarafa ya Shelui.
Alisema
mfanyakazi/dereva akibainika amebadilisha matumizi ya magari hayo ya
kubebea wagonjwa na kuanza kubeba mikaa, abiria au nafaka, ahesabu moja
kwa moja kwamba, amejifukuza kazi.
“Mkurugenzi
wa halmashauri husika naye akibainika kutowajibika kikamilifu kuhusu
kusimamia magari hayo yanatumika kwa lengo la kusafirisha wagonjwa tu,
nao watachukuliwa hatu akali za kisheria”,alisisitiza Dk.Kebwe.
Aidha,
Dk. Kebwe ambaye pia ni mbunge (CCM) wa jimbo la Sengerema, amewaasa
waganga wakuu wa halmashauri za majiji, Manispaa na wilaya, kusimamia
vizuri i matumizi ya madawa na vitendea kazi, ili huduma za afya ziweze
kukidhi mahitaji ya wananchi.
“Mganga
mkuu ye yote katika halmashauri atakayebainika kuzembea au kuruhusu
wizi wa dawa/vitendea kazi, atakuwa amepoteza sifa yake ya uganga mkuu
na hivyo italazimika kuchukuliwa hatua za ksiheria”,alisema.
Katika
hatua nyingine,Dk. Kebwe amewataka wananchi kuendelea na moyo wao wa
kuchangia maendeleo yao ikiwemo ujenzi wa nyumba za watumishi wa afya.
“Wananchi
wanalojukumu kubwa la kuchangia maeneleo yao ikiwemo kuhakikisha vituo
vya afya vinakuwa na nyumba za kutosha za kuishi watumishi.Bila nyumba
za kutosha kwa watumishi wentu wa sekta ya afya,tutakuwa tumetoa mwanya
watumishi kuweza kutukimbia”,alisema.
Wakati
huo huo, naibu waziri huyo alitumia fursa hiyo kumpongeza Naibu Waziri
wa Fedha Mwigulu Nchemba, kwa juhudi zake za kuwaondolea kero wananchi
wa jimbo lake ikiwemo kuwapa msaada wa Ambulance ambalo litawasaidia
hasa akina mama wajawazito kuwahi kwenye vituo vya afya.
Post a Comment