Kesi imefunguliwa katika Mahakama hiyo kwa
hatua za awali na upelelezi ukikamilika, itahamishiwa Mahakama Kuu
kuanza kusikilizwa.
Hakimu
Mkazi Waliarwande Lema alimnyima dhamana mshitakiwa huyo, kwa kuwa
mashitaka yanayomkabili hayana dhamana na Mahakama hiyo haina mamlaka ya
kusikiliza kesi hiyo.
Togbah anatuhumiwa Aprili 25, mwaka huu katika
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, aliingiza
gramu 862.3 za dawa hizo za kulevya zenye thamani ya Sh milioni 38.803.
Upande
wa mashitaka ulidai upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na kuomba
tarehe nyingine ya kutajwa ili wakamilishe upelelezi.
Mshitakiwa hakuruhusiwa kujibu mashitaka yake na kurudishwa rumande hadi Mei 12, mwaka huu, kesi hiyo itakapotajwa tena.
Post a Comment