
Hayo yamebainishwa wakati wa kutiliana saini ya mkataba wa maridhiano
kati ya NIMR na Kampuni ya UNHWA ya Jamhuri ya Watu wa Korea Kusini
iliyofanyika jana jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa NIMR, Mwele Malecela alisema utekelezaji wa makubaliano
hayo utaifanya Tanzania kuwa nchi ya kwanza kutumia teknolojia hiyo.
"Kwa sasa hali ya kiwanda chetu kwa upande wa vifaa haijakaa sawa, hivyo
tutachukua hatua katika kuhakikisha tunahamishia teknolojia hiyo hapa
nchini," alisema.
Alisema kwa sasa, taasisi yake itakuwa ikifanyia majaribio dawa
zinazotengenezwa na kampuni hiyo kwa kuyapa kipaumbele magonjwa ya
Ukimwi na saratani.
"Juzi wenzetu hawa walitembelea kiwanda chetu cha Mabibo na maabara na
wametupa moyo kuwa pamoja na kuwa ndio tunaanza tunaweza kufika mbali
katika kutengeneza dawa za binadamu kwa kutumia mimea.
Aidha, Malecela alimshukuru Rais Jakaya Kikwete kwa kufuatilia na kuunga
mkono juhudi za utafiti. Alisema teknolojia hiyo itasaidia Watanzania
kupata dawa bora na nzuri kwa kutumia mimea.
Mkurugenzi wa UNHWA, Youngwoo Jin alisema, "Kwa ushirikiano wetu tunaweza kupiga hatua katika hili."
Post a Comment