Kawaida ukiwa kwenye uhusiano wa muda mrefu zile chachu za mapenzi
hupungua kulingana na muda unavyokwenda.Kuna njia/mbinu tofauti ambazo
zinaweza kutumika kurejesha mihemeko ya mahabati
Kukumbatia kwa sekunde 20:
Kukumbatia/ana ni kitendo kinarejesha ukaribu wenza walio na mapenzi
yanayofifia.Ukikumbatiana kwa sekunde 20 mwili unaongeza production ya
oxycontin ambayo inaongeza ukaribu wenu.
Usafi na mpangilio chumbani:
Chumbani ni sehemu ambayo wenza wanakuwepo muda mwingi
wakihitajiana.Usiweke picha za familia kama mkweo au ndugu zako eneo
hili,ni vyema pia ukiepuka kuweka luninga chumbani.Vitu hivyo
vinapunguza mihemeko ya mapenzi mfano kama luninga inaweza kutumika kama
sababu ya kuepuka ukaribu.
Tuna ujumbe wa mahaba:
Mtumie ujumbe wa mahaba mwenza wako,kama iwe kwa njia ya barua
pepe,au ujumbe mfupi,ujumbe ambao utaamsha mhemeko wa mapenzi na
kuonesha hitaji lako kwake.
Mwambie unachokihitaji:
Ni vyema kama mwenza wako akijua vitu vipi unapenda na usivyopenda
na iwapo kama ametenda kitu usichokiridhia mjulishe na mwambie kile
unachokihitaji kutoka kwake.
Fanya yale yasiotarajiwa:
Maisha ya mahusiano yamejiegemeza kwenye uaminifu,matarajio fulani
kutoka kwa mwenza wako.Ni vitu vizuri vikihusishwa na economy ya familia
na utunzaji lakini si kwenye mahusiano.Fanya kile ambacho hutarajiwi
kukifanya kama "SURPRISE" mfano watoto wakishalala au asubuhi ukiamka.
Weka muda kwaajili yenu tu:
Panga muda utoke wewe na mwenza wako ili muwe faragha pamoja bila
bugudhi kutoka kwa watoto au watu wengine.Huu utakuwa ni muda muafaka wa
kukumbushia ya zamani.
Mfanye tendo la ndoa bila "tendo lenyewe":
Tendo la ndoa halihusishi mwili tu bali akili pia.Kuwa creative na
kumbambiana/kunyegezana na kufanya vitu ambavyo vinawaunga pamoja bila
kuhushisha kuingiliana kunaongeza chachu za mapenzi.
Ugomvi usifike chumbani:
Yale yote yanayofanyika nje ya chumbani yanaathiri yatakayotendeka
chumbani.Kama mna ugomvi,malizeni huo ugomvi kabla hamjaenda
kulala.Mkumbatie mwenza wako,mtanie au mpe busu la nguvu kama mna
mabishano yanayopelekea ugomvi.
Chunguza ayapendayo mwenza wako:
Fanya yale ambayo mwenza wako anayapenda kama kumpa compliment ili
kuongeza kujiamini kwake,msifie mumeo au mkeo kama ni mdada/mkaka mwenye
mvuto wa mahaba.
Fanya mazoezi au vile vitu unavyopendelea:
Jinsi unavyojitunza na kujijali mwili wako,ndivyo unavyokuwa katika
hali ya kujihisi una mvuto wa mahaba.Fanya vile vitu unavyovipenda ili
kujihisi una mvuto na kukuongezea kujiamini
Tembelea tena zile sehemu za fungate:
Kumbushia zile siku za furaha ambapo shamrashamra za mapenzi zilikuwa zimenoga,fanya hayo katika uhusiano wako wa sasa.
Post a Comment