Filamu ya kwanza ya Hollywood ilimpa Lupita Nyong’o tuzo ya
kwanza ya Oscar. Na sasa jarida la People limemtaja Mkenya huyo kuwa
ndiye ‘mtu mrembo zaidi duniani’ kwa mwaka 2014.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa uhariri wa jarida hilo, Jess Cagle
Nyong’o alikuwa chaguo sahihi kukava issue ya jarida hilo la kutimiza
miaka 25. “She is fantastic. There really was no contest this year. The
way she carries herself with such grace and humility, it put her over
the top. I just love her,” alisema. Jarida hilo liliwahusisha wasomaji
wake kutaja mtu anayestahili kuchukua heshima hiyo mwaka huu na Lupita
kupendekezwa na wengi.
Na sasa mrembo huyo ameungana na wanawake wengine waliowahi kukava
issue ya kutimiza mwaka wakiwemo Julia Roberts, Michelle Pfeiffer,
Beyonce Knowles, Drew Barrymore na Jennifer Lopez. Kwa miaka 25, jarida
la People limekuwa likitoa heshima hiyo na ni wanaume watatu tu
waliowahi kupata ambao ni Mel Gibson, Tom Cruise na Leonardo DiCaprio
(1996, 1997 na 1998). Mwaka jana alikuwa muigizaji Gwyneth Paltrow
Post a Comment