Ronaldo |
KLABU ya Real Madrid
imepata pigo kufuatia habari kuwa Cristiano Ronaldo anaweza akaukosa
mchezo wa fainali ya Kombe la Mfalme dhidi ya Barcelona wiki ijayo
kutokana na majeraha ya msuli.
Nyota huyo wa kimataifa wa Ureno alitolewa nje katika dakika za mwisho katika mchezo dhidi wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Borussia Dortmund ambao Madrid walishinda 3-0.
Majeruhi yamepelekea nyota huyo kupumzishwa katika mchezo wa La Liga dhidi ya Real Sociedad na alikuwa mchezaji wa akiba asiyetumika katika mchezo wa marudiano dhidi ya Dortmund ambao Madrid walichapwa kwa mabao 2-0.
Sasa imethibitika kuwa nyota huyo mwenye umri wa miaka 29 kwamba ameumia msuli wa paja la mguu wake wa kushoto na kuna uwezekano akakaa nje ya uwanja kwa kipindi cha wiki mbili hivyo kuukosa mchezo huo wa muhimu wa Kombe la Mfalme Jumatano ijayo.

Post a Comment