Selena Gomez amrudia Mungu kuepuka rehab

Selena Gomez ameamua kumrudia Mungu kwa kuanza kwenda kanisani mara kwa mara ili kuepuka kurejea tena rehab kwa matatizo ya msongo mkubwa wa mawazo.
Selena-Gomez-Photoshoot-Pictures-Wallpaper-Selena-Gomez
Chanzo kimoja kimeuambia mtandao wa HollywoodLife.com: “Selena anajaribu kubadilisha maisha yake kwa kwenda kanisani kuepuka kwenda rehab. Anahisi kuwa ana gap la kiroho na kwamba ndio maana anapata tabu.”
Muimbaji huyo wa ‘Come & Get It pia ameamua kuachana na kampani yote anayohisi ni chanzo cha mabaya kwakuwa anataka kujikita katika career yake zaidi. Mrembo huyo anadaiwa kumpiga chini mpenzi wake Justin Bieber wiki iliyopita baada ya kugundua kuwa hajatulia.
Miongoni mwa marafiki alioachana nao ni wadogo zake Kim Kardashian, Kendall na Kyle ambao amewaunfollow wote kwenye Instagram.

Post a Comment

Previous Post Next Post