
Leo
Jumatatu, Aprili 7, Redio yako ya Kijamii ya KwanzaJamii imeandika
historia kwa kuwa redio ya kwanza hapa nchini kuwaletea wasikilizaji
dondoo za habari za magazetini kutokea kwenye soko lenyewe la habari,
ni pale kona ya Uhuru na Msimbazi, Kariakoo.
Ni
kipindi cha kila siku kuanzia saa kumi na moja na nusu alfajiri.
Mwandishi/ Mtangazaji wa KwanzaJamii atakuwa sokoni hapo na kuungana
moja kwa moja na studio za Kwanzajamii radio Iringa.
Sambamba
na redio, habari hizo na picha za magazeti yenyewe zitarushwa pia
kwenye Mjengwablog.com. Ikumbukwe, Mjengwablog ilikuwa ni blogu ya
kwanza hapa nchini kuanza kurusha kwenye blogu dondoo za magazetini.
Usikose kufuatilia na kuzipata habari zikiwa motomoto kutoka Soko la habari Kariakoo…http://www. mjengwablog.com/habari-za- kijamii/item/10489-kutoka- soko-la-habari-kariakoo.html#. U0JH6ldQ7U4
Post a Comment