
Mnamo
mwaka 2010 kampuni ya magari nchini marekani ijulikanayo kwa jina la
TESLA MOTORS, ikiongozwa na CEO Elon Musk ambae akiwa kwenye mkutano na
wafanyakazi aliinua glass ya Champagne na kuwambia wafanyakazi wake kuwa
ni muda wa kutengeneza kampuni ya gari ya karne ya 21 ambayo italeta
tofauti kubwa duniani, ambayo itatuondoa kwenye matatizo ya OIL kabisa.
vile vile unaweza ukamuangalia Musk katika Documentary ya dakika 80
inayojulikana kama “Revenge of the Electric Car”, CEO Elon MUSK ambae miaka 17 ya maisha yake amekulia nchini SOUTH AFRICA alisema…….


TESLA Model S ni gari ambayo haitumii mafuta na wala haina Engine, gari hii haina mlio wala kele za aina yoyote na inachokatiwa kufanyika ni kuchaji battery ambayo imetengeneza ndani ya gari upande wa chini wa chasis na kuendesha tu. gari za aina hii zimeshaanza kutumika nchini AMERICA ambapo mtanzania RAK Baraka aishie nchini humo ambae amekua mmoja ya watu ambao wamekua wa mwanzoni kuendesha gari ya aina hiyo alisema…

“Nomaaa Mwanangu, nikisema Nomaa yani I mean Nomaa….. yani nimeendesha nimeenda kulipaki kwenye Shopping Mall, kuna Parking zake special ambazo zina kampuni ya kuchaji inakuja kulichaji”… aliendelea kusema “Computer system ya humo ndani ni balaa na halina sound kabisa” alisema Baraka RAK CEO, AMANI Clothing Company.

Gari hii vitasa vyake vina “sensor” ambapo ukisogeza mkono vitasa ndio vinatoka… Gari hizi ambazo zimetoka muda kidogo, sasa ndio zinaanza kusambaa sehemu nyingi hata nchini uingereza ukienda kwenye mahospitali kama Royal Free Hospital na Finchley Memorial Hospita mjini London Uingereza utakuja mashine hizo.

Kwanza kabisa Tesla walianza kutengeneza magari madogo kwa ajili ya matajiri na yanayotumika kwenye Golf “TESLA ROADSTAR” ambazo zilikua na thamani ya dola za kimarekani $109,000 ambazo alikua akiuza kwa watu wachache kwa mpango wa kukamilisha lengo lake la kutenegeza ‘Sports Cars’ kuuza na kutengeneza gari za kima cha chini ambazo kila mwananchi atakua na uwezo wa kununua na kutumia. Gari hiyo ambayo kwa sasa inapatikana kwa Dola za kimarekani $49,000 ambayo ni nusu ya ile aliyokuwa anauza ROADSTAR na CEO huyo amesema yupo mbioni haraka iwezekanavyo iweze kushuka mpaka dola za kimarekani $30,000.
Post a Comment