
Wapiganaji wa Ukraine wanaounga mkono Urusi
Waziri wa mambo ya nje wa Urusi,
Sergei Lavrov, ametuhumu maafisa wakuu wa Kiev kwa kuvunja mkataba
uliofikiwa wiki jana mjini Geneva kusuluhisha mgogoro wa Ukraine.
Alisema kuwa serikali ya Muda ya Ukraine ,
ambayo haitambuliwi na Moscow, haijachukua hatua zozote kuwapokonya
silaha makundi haramu hasa wapiganaji wazalendo.
"wapiganaji wenye itikadi kali ndio
wenye kauli kuu,'' alidai waziri huyo akilaani kitendo cha mashambulizi
yaliyotokea Mashariki mwa Ukraine.
Pia alilaani maandamano yanayoendelea katika barabara ya Maidan mjini Kiev.
Mapema Jumapili, watu watatu waliuawa baada ya
kushambuliwa kwa bunduki katika kizuizi cha barabarani kinachodhibitiwa
na wapiganaji wa Ukraine wanaounga mkono Urusi.

Ukraine imedaiwa kutositisha ghasia
Hali iliyosababisha tukio hilo bado
haijajulikana. Watu wanaotaka kujitenga na Ukraine walisema kuwa
shambulizi hilo lilifanywa na wapiganaji wazalendo wa Ukraine.
Mkataba unavyokiukwa
Hata hivyo serikali ya Ukraine ilitaja shambulizi hilo kama uchokozi unaofanywa na wanajeshi wa Urusi.
Tarehe 17 mwezi Aprili, mkataba wa Geneva,
ulifikiwa katika mazungumzo yaliyoshirikisha Urusi, Ukraine na Muungano
wa Ulaya na Marekani.
Mkataba huo ulitoa wito wa kusitishwa kwa ghasia
Mashariki ya Ukraine na kutoa wito kwa makundi haramu kusalimisha
silaha zao na kuondoka kutoka majengo ya serikali.
Wapiganaji wanaounga mkono Urusi, bado
wanadhibiti majengo ya serikali katika miji tisa katika jimbo la Donetsk
mashariki mwa Ukraine.
Bwana Lavrov alisema ombi kubwa la makubaliano
ya Geneva lilikuwa kuzuia ghasia zozote, lakini ombi hilo halizingatiwi
na Ukraine.
- Bbc
Post a Comment