Urusi yatumia kawi kuishurutisha Ukraine.

Kawi ya gesi inatumiwa na Urusi kama silaha ya kuishurutisha Ukraine.
Marekani imelaani kile imekitaja kuwa hatua ya Urusi kutumia kaiwi kama chombo cha kuishurutisha Ukraine.
Msemaji wa wizara ya mashauri ya nchi za Kigeni, Jen Psaki, amesema bei ambayo Ukraine inalazimika kuilipa Russia kununua gesi haijaamuliwa na mahitaji pamoja na kanuni za soko.
Hatua ya Urusi kuongeza maradufu bei ya gesi inayouzia Ukraine imeudhi mataifa ya Magharibi ambayo sasa yameanza kulalamikia kile yanasema Urusi kutumia rasilmali muhimu kama hiyo kulazimisha taifa hilo dogo lililo jirani yake kukubaliana na mipango yake ya kuendelea kumegua eneo lake kuwa sehemu ya Urusi.
Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni wa Marekani, Jen Psaki, amesema kuwa ongezeko la bei ya gesi inayouziwa Ukraine na Urusi kwa sasa halikutokana na shinikizo la soko.
Gesi kutoka Urusi
Alisema Marekani itatoa msaada wa kifundi kuhakikisha kuwa Ukraine inapata gesi inayohitaji. Marekani pia imesema itaomba mataifa ya Magharibi kurejeshea Ukraine gesi ambayo ingali katika mabomba yake yanayopitia Ukraine ili taifa hilo lipate gesi inayohitajika kwalo.
Taarifa ya Bi Psaki imetolewa muda mfupi baada ya Rais wa Urusi Vladmin Putni kuandilia barua viongozi wa Mataifa ya Jumuiya ya Ulaya kuwa gesi wanayopokea kupitia mabomba yanayopitia Ukrain huenda ikakatwa kutokana na deni kubwa la Ukraine kwa Urusi.
Kampuni kubwa ya Nishati ya nchini Urusi, Gazprom, imesema kuwa inadai Ukraine Dolar Bilioni Mbili Nukta Mbili.
Kutokana na barua hiyo ya Rais Putni, Rais Obama wa Marekani amewasiliana kwa simu na Chanselar wa Ujerumani Angela Merkel, juu ya uwezekano wa gesi inayopitishiwa Ukraine kusitishwa. Mataifa mengi ya Magharibi huagiza kiasi kikubwa cha gesi kutoka Urusi kupitia Ukraine.

Post a Comment

Previous Post Next Post