DOGO MASAI ni filamu nzuri ya kitanzania inayomzungumzia kijana
mdogo JAMES ambaye anaamua kuuvaa muonekano wakimasai baada ya kufanyiwa
dhuluma na mjomba wake (Tino) na kisha kutupwa porini ambapo aliokotwa
na WAMASAI.
https://www.youtube.com/watch?v=gyemmaw4x
Ni filamu yakusisimua hasa kutokana na vituko vya DOGO MASAI ambapo
anaingia mjini na kuhangaika kuzitafuta mali ambazo alidhulumiwa na
kuishia mtaani akiranda randa na kuomba msaada hapa na pale.
“FIlamu hii kabla hata ya kutoka tayari imeshaonyesha mwanga fulani,
nitakujuza hivi karibuni baada ya kufanikiwa kwa mipango ya kuipeleka
filamu hii kimataifa zaidi,” amesema Timoth Conrad wa kampuni ya Timamu
African Media ambaye ni mwandishi, muongozaji na mtayarishaji wa filamu
hiyo.
Washiriki katika filamu hiyo ni pamoja na TINO MUYA, OMARY CLAYTON,
JAMES SAMALE, MUKASA TABANI, MAINDA SUKA, JULIETH SAMSON (KEMY).
Tazama baadhi ya picha zake hapa.



















Post a Comment