SI msela tena imethibitishwa na wanasheria wake kwamba anataka sasa
kutoka rasmi na Amal Alamuddin.Ameingia katika mahusiano hayo wakati
mwaka Mwaka 2007, alisema kwamba hataoa tena.
|
kifaa cha sasa kinachoenda kufunga ndoa amal-alamuddin |
Sina mpango wa kueleza maisha yake ya usela, akiwa anajulikana kwamba ndiye bachela wa muda mwingi katika maeneo ya Hollywood.
Akiwa
amezaliwa Mei 6, 1961 Clooney ambaye ni muigizaji, dairekta, projuza na
mwandishi wa skrini ameshatunukiwa tuzo tatu za Golden Globe kwa kazi
zake na mbili za oscar moja kw auigizaji na nyingine kwa kuprojuzi.
Msela
huyu ambaye ni mjumbe wa amani wa Umoja wa Mataifa kuanzia januari
31,2008 alianza shughuli za uigizaji kw anjia ya televisheni mwaka 1978
kama Dk. Douglas "Doug" Ross katika kipindi cha televisheni cha ER
kuanzia 1994 hadi 1999, ambako pia alishawishi watu kutuma jina la
kuwania tuzo za Emmy.
|
akiwa na elisabetta |
|
akiwa na kelly-preston |
|
akiwa na Talia |
|
akiwa na kimberly |
|
akiwa na celine |
|
akiwa na Lisa |
|
akiwa na renee |
|
akiwa na krista |
|
akiwa na sarah-larson |
|
akiwa na stacy-keibler |
|
akiwa na monika-jakisic |
Pamoja na mafanikio yake katika uigizaji na uongozaji mwaka 2005, TV
Guide ilisema kwamba Clooney ni namba moja miongoni mwa mastaa wenye
mvuto wa kimapenzi 50 kwa muda wote.
Clooney akiwa amezaliwa
Lexington, Kentucky, mwaka 1961 kutoka kwa mama Nina Bruce (née Warren,
1939–) na baba Nick Clooney amekuzwa katika sheria madhubuti za kanisa
Katoliki. Alikuwa mtumishi wa altareni.
Mtumishi huyu wa
altareni alioana na muigizaji Talia Balsam kuanzia mwaka 1989 na
kuachana 1993 hakuwai kuoa tena na badala tajke amekuwa katika mahusiano
na wanawake kadhaa.
Alikuwa na uhusiano na muigizaji Ginger Lynn
Allen na baadae akawa na mwanamitindo wa kiingereza Lisa Snowdon mwaka
2000.Alikuwa na uhusiano wa njoo na uende kwa miaka mitano na binti
huyo.Juni 2007,alianzisha uhusiano na Sarah Larson, lakini Mei 2008
waliachana.
Julai 2009, Clooney aliingia katika uhusiano na
muigizaji wa Kitalia, Elisabetta Canalis na kuachana naye Juni 2011 na
kuanzia Julai 2011, Clooney alianzisha uhusiani na WWE Diva, Stacy
Keibler,na kukatisha uhusiano wao Julai 2013.
Katika maisha yake
Clooney ameshawahi kuwa na uhusiano pia na Kelly Preston (1987–1989),
Renée Zellweger (2001) na Krista Allen (2002–2008) pia na Céline
Balitran (1996–1999).
Post a Comment