![]() |
| Meneja Uhusiano wa Nje wa Kampumi hiyo, Salum Mwalim |
Mdhamini Mkuu wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania, wameipongeza timu ya Azam FC kwa
kufanikiwa kutwaa ubingwa wa ligi hiyo kwa msimu wa 2013/2014 ikiwa ni Mara ya kwanza tangu kuanzishwa kwake miaka 7 iliyopita.
kufanikiwa kutwaa ubingwa wa ligi hiyo kwa msimu wa 2013/2014 ikiwa ni Mara ya kwanza tangu kuanzishwa kwake miaka 7 iliyopita.
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa mechi
kati ya Mbeya City na Azam FC kwenye uwanja wa Kumbukumbu ya sokoine
mjini Mbeya Meneja Uhusiano wa Nje wa Kampumi hiyo, Salum Mwalim amesema
wakiwa wadhamini wameridhishwa na kiwango cha Azam FC pamoja na timu
zote zinazoshiriki katika ligi na hivyo wanawapongeza kwa dhati timu
hiyo kwa kuibuka mabingwa.
“Tunachukua nafasi hii kuwapongeza Azam kwa kuwa bingwa mpya wa
Vodacom Premier League (VPL) 2013/2014,wamekabiliana vema na
mikikimikiki ya ligi na hivyo ubingwa wao haukuwa mwepesi kuupata
kutokana na ushindani uliokuwepo kwa timu zote shiriki,” alisema Mwalim.
“Tumeifuatilia ligi na tunaimani kuwa Ligi imetoa bingwa aliyestahili
na ambae yupo imara kutokana na kupitia safari ndefu na ngumu ya ligi na
ni imani yetu kwamba atakuwa mwakilishi mzuri kwenye michuano ya klabu
bingwa Afrika akiitangaza nchi na
pia Vodacom Premier League.”
pia Vodacom Premier League.”
Mwalim amesema Azam inabeba kwa mara ya kwanza ubingwa wa ligi tangu
timu hiyo ilipoanza kushiriki ligi kuu mmwaka 2008 na kwamba ushindi huo
bila shaka utaongeza ushindani kwenye msimu ujao.
“Ubingwa wao huenda ukaifanya ligi ya mwakani kuwa ngumu zaidi kwani
timu za Yanga na Simba ambazo zimekuwa zikipokezana ubingwa kwa
takribani miaka 20 zitataka kurudisha heshima yao na nyengine zikipata
nguvu kuwa yoyote anaweza kuwa bingwa iwapo atajipanga vema kumudu
ushindani,hilo likitokea ubora wa ligi yetu utazidi kupaa”Alisema Mwalim
Amesema Azam watakabidhiwa kombe lao la ubingwa April 19 kwenye
uwanja wa nyumbani Chamazi wakati wa mechi yao ya mwisho dhidi ya JKT
Ruvu. Akizungumzia ligi, Mwalim amesema ilikuwa ya ushindani mkubwa na
takribani kila mechi ilikuwa ngumu kwa kila timu hali iliyolazimisha
hata bingwa kujulikana kwenye mechi za mzunguko wa mwishoni.
“Tumefika mahali tunapoweza kuzungumza mazuri zaidi kuhusu ligi
tofauti na tulikotoka,ni wazi kwamba ligi yetu imepiga hatua na Vodacom
kama mdhamini Mkuu tutaendelea kufanya kila lililo ndani ya uwezo wetu
kuimarisha ubora huo,” alisema Mwalim.
Aidha Mwalim amezipongeza timu zote 14 zilizoshiriki ligi hiyo kwa
kujituma na kutoa changamoto katika kila mechi jambo lililofanya bingwa
kutopatikana kwa urahisi na mapema. Aidha amezipongeza timu za Yanga na
Mbeya City kwa kuwa katika msimamo wa kumaliza
kwenye nafsi ya pili na ya tatu huku akiitaja timu ya Mbeya City kuwa ni timu iliyoleta changamoto mpya kwenye ligi na kuipa afya zaidi ligi hiyo.
kwenye nafsi ya pili na ya tatu huku akiitaja timu ya Mbeya City kuwa ni timu iliyoleta changamoto mpya kwenye ligi na kuipa afya zaidi ligi hiyo.
“Mbeya City wamecheza vizuri sana tangu mwanzoni mwa ligi hadi
wanapoelekea kumaliza mchezo wao wa mwisho wa ligi,wameonesha mfano kwa
timu zinazopanda daraja nanmna gani wanavyoweza kuwa timu shindani
badala ya kuwa timu shiriki, aliongeza.
Alisema awali ilionekana kuwa ni nguvu ya soda lakini kadiri ligi
ilivyokuwa ikosonga mbele ilionesha kuwa imedhamiria kufanya vema huku
ikihimili mikikimiki yote ya ligi kuu na hivyo kuifanya kuwa timu
inayohitaji kupewa sifa za kipekee kwa msimu huu.
Vodacom imewapongeza pia wakazi na wenyeji wa mkoa wa Mbeya kwa
kuiunga mkono timu yao kwa hali na mali na hivyo kuipatia mafanikio huku
hatua yao hiyo ikinogesha pia joto la ligi ndani na nje ya mkoa wa
Mbeya.

Post a Comment