Kwa mujibu wa mashuhuda wa mkasa huo wafanyakazi hao wa kambi ya
ujenzi ya Kianda wilayani Sumbawanga walileta usumbufu mkubwa
wakipinga walinzi wa kampuni hiyo kumkamata opereta wa tingatinga,
aitwaye Gabriel Daniel (34) mkazi wa eneo la Bomani , Manispaa ya
Sumbawanga.

Wafanyakazi hao walifunga barabara wakipinga kitendo cha walinzi wa
kampuni hiyo kumzuia mwenzao mmoja wakimtuhumu kutaka kuiba mafuta.
Kufuatia dhahama hiyo wafanyakazi hao wenye hasira waliteketeza
kwa moto magari makubwa manne. Magari hayo ni pamoja na Scania
Tipper lenye namba za usajili T 755 CAV, Iveco lenye namba za usajili
T 116 AYT , gari aina ya Artego lenye nambari za usajili T 839 na
gari aina ya Artois yenye namba za usajili T 936.
Watu wawili wanashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kuhusika na tukio
hilo.Watuhumiwa hao ni Emanuel Sanga (34) mkazi wa Mkoa wa Iringa na
Ngasa Mathias (40) mkazi wa wilayani Chunya, Mbeya.
Post a Comment