
Baadhi ya
viongozi wa jamii ya Wasomali Kenya na viongozi wa Kislamu wamelaani
msako mkubwa unaofanya na polisi na kikosi maalum cha kupambana na
ghasia mjini Nairobi kufuatia mashambulio na mauwaji ya hivi karibuni
huko Kenya.
Viongozi
hao wameituhumu serikali kwa kuwalenga Waislamu na hasa Wasomali
walipofanya msakao mkubwa wa nyumba moja hadi nyingine katika mtaa wa
Eastleigh mwishoni mwa wiki na kuwakamata karibu watu 500.
Mwishoni
mwa wiki katika msako mkubwa ulowahusisha karibu polisi elfu sita na
wale wa kikosi maalum cha kupambana na ghasia ulifanyika ili kuwasaka
mahalifu kufuatia miripuko mitatu ya bomu mjini Nairobi wiki ilyopita.
Mkuu wa
wabunge waliowengi Aden Duale mwenye asili ya Kisomali alikua afisa wa
kwanza kutishia siku ya Ijuma kwamba atajiondoa kutoka mungano
unaotawala wa Jubilee, kutokana na kile alichokieleza ni "kukamatwa
kiholewa wakazi wa jamii yake."
Siku ya
Jumapili viongozi wa jamii ya Kislamu na Wasomali, walikutana Nairobi na
wamelaani kitendo cha polisi kuwakamata na kuwabughudhi watu wakati wa
msako wa mtaa wa Eastlegh.
Akizungumza
na Sauti ya Amerika mbunge wa Mvita, Mombasa, Abdulswamad Sharif Nassir
anasema, msako huo unaowalenga jamii fulani ya watu ni makosa na
inazidisha chuki miongoni mwa wakazi.
Waislamu Kenya walaani misako ya kiholela
Waislamu Kenya walaani misako ya kiholela
Naibu
Spika wa zamani wa bunge la Kenya Farah Maalim, kwa upande wake alisema
Jumapili, kwamba polisi wamewaibia raia na kuwabughudhi na kuwakamata
wanawake na watu wasohusika na ugaidi.
Mwambi
Mwasaru, Mkurugenzi wa kundi la kutetea haki za waislamu Mombasa,
Muhuri, anasema polisi wanakiuka haki za binadam na sheria za nchi
wanapofanya msako jumla na kwa njia ya kiholela.
Bw
Mwasaru anasema makundi ya kutetea haki za binadam yanaitaka serikali
itafute mbinu nyingine kuwasaka magaidi na wala si raia wasio na hatia.
Lakini
inavyonekana hadi hivi sasa wakuu wa usalama wanatetea mbinu wanaotumia
kwani kamishna wa polisi wa County ya Nairobi, Njoroge Ndirangu anasema
hawajalenga Eastleigh pekee, bali ni msako uloanza mwezi Februari na
utafanyika Nairobi nzima.
Kutokana
na msimamo huo Mkurugenzi wa Muhuri anasema watalazimika kufikisha
mashtaka mahakamani. Mbunge Sharif Nasser kwa upande wake anasema
inabidi kuwepo na mazungumzo kati ya pande zote zinazohusika ili
kukabiliana na tatizo jumla la usalama.(Hudugu Ng'amilo)
CHANZO SAUTI YA AMERIKA
CHANZO SAUTI YA AMERIKA
Post a Comment