Hii inaweza kuleta ugomvi wa fikra kati ya uhalisia na
utafiti wa wanasayansi katika dunia hii inayoendeshwa na mambo mengi
yaliyogunduliwa na wanasayansi, lakini…amini usiamini hiki ndicho
kilichoonekana kwenye vipimo vyao.
Wanasayansi wa chuo cha West Manchester cha Uingereza ambao wamebobea
kwenye masuala ya saikolojia na biology, wametumia kipimo cha vinasaba
‘DNA’ kufanya utafiti uliohusisha saikolojia na biology ya binadamu na
kugundua kuwa karibu wanaume wote wanachepuka katika mahusiano yao.
Wanasayansi hao wamekuwa wakifanya utafiki wa vinasaba kwa makundi
mbalimbali ya wanaume kwa lengo la kufahamu utofauti wa kisaikolojia
kati ya wanaume na wanawake katika mahusiano.
Kwa mujibu wa utafiti huo ulioripotiwa na mtandao MapeNation uliopata
copy iliyokusudiwa kupelekwa kwenye vyombo vya habari, wanasayansi hao
walitumia vipimo vya vinasaba vinavyopatikana katika meno makali ya
mbele ya mbwa ‘canine teeth’ ambayo yameelezwa kutumika katika kuzalisha
madini ya proteins na nucleic acids, ambazo huongeza hali ya mbwa
kutaka kuwa na mwenza wake kwa kiwango cha juu.
Baada ya majaribio kadhaa, walihitimisha kuwa takribani miaka 200,000
iliyopita aina ya mbwa aina wenye meno makali walikuwa wakiwinda
wanyama kwa ajili ya chakula. Kadri muda ulivyozidi kwenda wanyama hao
walitengeneza vinasaba ambavyo vinaendana na vile vya wanyama hao
waliokuwa wakiwawinda na kuwala, na vina hivyo vilitumika kama kinga
dhidi ya wanyama wenzao wanaowala (predators).
Imeeleza kuwa wanyama hao waliotengeneza vinasaba hivyo walivyozidi
kusambaa na kujikuta wakiliwa na binadamu wa sasa. Na mwisho binadamu
hao wameendelea kubeba vinasaba vinavyobeba virutubisho vilivyozalishwa
na wanyama hao (biopolymer).
Matokeo yake, binadamu (wanaume) walirithi vitu vinavyosababisha
msukumo/khari ya kutaka kuwa na wenza hali inayowapelekea kusaka
wanawake kadri iwezekanavyo wakati huo.
Mwandishi wa mtandao wa MapeNation aliyejitambulisha kwa jina la Zay
alimuomba Dr. Yus I. Birchmier atoe ufafanuzi rahisi kuhusu utafiti huo
na akaeza kuwa inaonesha kuwa tabia ya kuchepuka aka kusaliti kaika
uhusiano wa mapenzi iko kwenye vinasaba vya mwanaume.
“Well, essentially, it means that it is in a man’s DNA to cheat. It
can no longer be denied. The DNA links prove it.” Alieleza Dr. Yus.
Hata hivyo, walipoulizwa wanaume kadhaa kuhusu majibu hayo wengi walionekana kuchukizwa nayo huku baadhi wakiyafurahia.
“It’s bullsh-t! It’s just another thing for females to throw in our
face! They should have kept this sh-t secret!” alisema Clyde Williams.
Matokeo ya utafiti huo yanatarajiwa kutangazwa rasmi wiki kadhaa zijazo.
Post a Comment