
WANAUME wametajwa kuwa chanzo kikuu cha wanawake kupata ugonjwa wa saratani ya mlango wa uzazi ambayo imekuwa tishio kwa sasa.
Mshauri
wa Shirika lisilokuwa la kiserikali la PSI-Tanzania, Dk. Mashafi Joseph,
alieleza hayo jijini Dar es Salaam juzi alipozungumza na waandishi wa
habari akizungumzia udhamini wao katika Jukwaa la Wanawake la 'Familia
Kitchen Party Gala', litakalofanyika Aprili 27, katika Ukumbi wa Diamond
Jubilee kupitia chapa yao ya familia.
Akifafanua
hilo, Dk. Mashafi alisema kisayansi wanaume ndio wabebaji wa kirusi
kinachosababisha ugonjwa huo kinachoitwa Human Papillomavirus (HPV)
ambako kwao hakina madhara ila kinapofika kwa mwanamke ndipo anapata
saratani hiyo ambayo huambukizwa kwa njia ya kujamiana.
Kwa hapa
nchini alisema saratani hiyo si tu inaongoza kwa vifo vya kina mama bali
pia ni aina ya saratani ambayo inakuwa kwa kasi katika nchi za Afrika
Mashariki huku Tanzania ikiwa na mzigo mkubwa wa wagonjwa.
Kuhusu
udhamini wao kwa jukwaa la 'Familia Kitchen Party Gala', inayoandaliwa
na Women Footprints Initiative, alisema wameamua kushirikiana nao kwa
lengo la kupunguza vifo vya kina mama vitokanavyo na uzazi.
CHANZO TANZANIA DAIMA
CHANZO TANZANIA DAIMA
Post a Comment