Timu ya Didi’s Bar imeibuka na ushindi wa michuano ya Foosball Tanzania inayoandaliwa na bia ya Heineken.
Mkurugenzi mkuu wa Heineken Tanzania, Uche Unigwe wa kwanza
Kushoto, na wachezaji wa Didi’s Bar, Ntoli Mwaikambo na Eric Duncan
pamoja na mmiliki wa baa hiyo iliyopo Masaki, Hillary Marc Mremi
wakipokea chekiJumla ya timu 6 zilishindanishwa kwenye michuano hiyo. Timu zingine zilizoshiriki ni pamoja na Hisaje park, Kwetu Pazuri, Catalunya, Corner Bar, Kisuma Bar, Nanuku, Samaki Samaki city centre, Uhuru Peak, Amsterdam Bar, Frisha’s Arena, Maisha Club, Igosi Lounge, Brazil, Jackie’s na Liquid bar.
Wachezaji wa timu ya Didis, Eric Duncan Lissa (wa kwanza
kushoto) akiwa na mwenzake Ntoli Mwaikambo wakichuana vikali na Said
Duche (wa kwanza kulia) na Abdala Kassim wa Hasadam , katika fainali ya
soka ya mezani ‘foosball’ iliyofanyika katika ukumbi wa Club 777 uliopo
Kawe, Dar es salaam. Timu ya Didi’z iliibuka kidedea kwa magoli 9-3 na
hivyo kushinda nafasi ya kwenda Ibiza Hispania kwa udhamini wa
Heineken foosball
Mkurugenzi mkuu wa Heineken Tanzania, Uche Unigwe alisema kuwa
mchakato wa Heineken kuwapata washindi ulikuwa wa aina yake kutokana na
ushindani ulioonyeshwa na timu zote zilizoshiriki.
Mkurugenzi mkuu wa Heineken Tanzania, Uche Unigwe akiongea na waandishi wa habari
“Baada ya mchakato wa kuwatafuta washindi hatimaye tulipata timu 2
ambazo zilishiriki kwenye fainali na kupata washindi ambao
watagharamiwa kila kitu katika ziara watakayoenda kufanya huko kisiwa
cha Ibiza, Hispania,” alisema. Washindi na wageni waalikwa kutoka nchi
mbali mbali watajumuika pamoja kusherehekea usiku mashuhuri wa
mashindano ya mpira wa miguu wenye hadhi ya kimataifa na Heineken.

“Foosball ambayo inachezwa na mashabiki wengi Ulimwenguni, umekua kati ya michezo inayokua zaidi kila siku na hivyo tumeamua kudhamini michuano hiyo tena kwa mwaka huu ili kuendelea kuongeza mashabiki wa soka ” alisema.
“Tunafurahia kuendelea kuona mchezo huu unazidi kukua hasa katika
nchi za Afrika Mashariki, kutokana na kuendelea kupata mashabiki wengi
zaidi kila mwaka, hivyo Heineken itaendelea kudhamini michuano ya
foosball,” alisema
Post a Comment