Mlipuko
wa bomu kwenye mji wa Arusha kwenye bar iitwayo Arusha Night Park
Mianzini April 13 2014 umesababisha watu 15 kujeruhiwa na kulazwa katika
hospitali tatu tofauti mkoani humo.
Waziri wa mambo ya ndani amethibitisha kujeruhiwa kwa watu lakini
hakuna kifo kilichotokana na mlipuko huo ambao uchunguzi wa awali
umeonyesha ni wa bomu la kutengeneza kwa mkono.
Waziri anasema >> ‘Mshambuliaji
alilitengeneza kwa kuchukua chupa ya Whisky iliyotumika na kuweka
utambi na vitu vingine kisha mfuko wa plastick wenye misumari alafu
akalitegesha ndani ya Bar hiyo iliyokua imejaa watu wakitazama mpira saa
mbili usiku’
Unaambiwa kabla ya bomu kulipuka, alietegesha bomu hilo ambae mpaka
sasa uchunguzi ukiendelea hajafahamika, alihamia kwenye Bar ya jirani
iitwayo ‘Washington’ na kutegesha bomu jingine la kienyeji ambalo hata
hivyo halikulipuka.
Wahudumu wa bar ya ‘Arusha night park’ wamesema wakati wa mlipuko huo
waliona kwanza mwanga mkubwa na moshi kujaa ambapo wenzao wameumia sana
ikiwemo kuvunjika miguu huku wateja baadhi wakiumia pia walipojaribu
kukimbia kutoka kwenye eneo la tukio.
Post a Comment