Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Mbarawa afungua mkutano wa wadau waTEHAMA

01

Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa akifungua mkutano wa siku mbili wa wadau  wa Teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA) kutoka nchi za ukanda wa Bonde la ufa leo jijini Dar es salaam. 
Na Eleuteri Mangi- Maelezo
Serikali imejenga mazingira mazuri kwa wawekezaji ili kuvutia makampuni mbalimbali kuwekeza kwenye sekta ya mawasiliano nchini.
Kauli hiyo imemtolewa na Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa alipokuwa akifungua mkutano wa siku mbili wa wadau Teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA) kutoka nchi za ukanda wa Bonde la ufa leo jijini Dar es salaam.
“Nawasihi wajasiriamali katika mambo ya TEHAMA ndani ya nchi washirikiane na wenzao wa nje ya nchi ili waweze kujijengea uwezo wa kukuza uchumi wa nchi yetu” alisema Prof. Mbarawa.
Prof. Mbarawa aliwasihi washiriki wa mkutano huo kuwa Tanzania inawakaribisha wawekezaji kuja kuwekeza katika TEHAMA ili kuhakikisha Watanzania wote wanapata huduma ya mawasiliano katika maeneo yote nchini hadi vijijini.
02
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia John Mngondo (kulia) akiwa miongoni mwa washiriki wa mkutano wa siku mbili wa wadau Teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA) kutoka nchi za ukanda wa Bonde la Ufa leo jijini Dar es salaam.
Aidha, Prof. Mbarawa alizitaja changamoto zinazoikabili sekta ya TEHAMA ni pamoja na ukosefu wa nishati ya umeme vijijini, kumudu gharama za uendeshaji, ukosefu wa vifaa vya sekta hiyo na usalama wa taarifa mbalimbali katika mitandao.
Kwa upande wake Waziri wa Mawasiliano, Habari na Uhusiano wa Bunge kutoka Burundi, Tharcisse Nkezabahizi alisema kuwa TEHAMA ni moja ya Nyanja muhimu inayotumiwa katika nchi yake ikiwemo elimu na huduma za afya ambapo ni muhimu kwa nchi za bonde la ufa kutumia teknolojia hiyo ili kukuza uchumi wan chi husika.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Digital Network Oy nchini Finland, Cipa Ojala alisema kuwa mkutano huo umekuja wakati mwafaka ambapo nchi nyingi zinatumia fursa iliyopo ili vyombo vya habari ikiwemo televisheni kuhama kutoka analogia kwenda dijiti.
Tanzania mpaka sasa imekuwa miongoni mwa nchi zinazofanya vizuri katika kutekeleza hatua ya kuhama kutoka mfumo wa analogia kwenda dijiti mbapo hadi kufikia mwishoni mwa mwaka huu takribani mikoa yote itakuwa imezima mitambo ya analojia kwenda dijiti.
Nchi zinazoshiriki katika mkutano huo ni Burundi, Rwanda, Somaliland, Zambia, Sudani Kusini ikiwemo Tanzania ambayo imekuwa mwenyeji wa mkutano huo kwa mara ya pili mfululizo pamoja na wadau wengine katika sekta hiyo.
03
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Digital Network Oy nchini Finland, Cipa Ojala akisisitiza umuhimu wa mkutano wa wadau wa TEHAMA katika nchi za Bonde la Ufa na msatakabali wa vyombo vya habari ikiwemo televisheni kuhama kutoka analogia kwenda dijiti.
04
Baadhi ya washiriki wa mkutano wa wadau wa TEHAMA kutoka nchi za Bonde la Ufa wakimsikiliza Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa (hayupo pichani) akifungua mkutano wa siku mbili wa wadau Teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA) kutoka nchi za ukanda wa Bonde la ufa leo jijini Dar es salaam.
05
Baadhi ya washiriki wa mkutano wa wadau wa TEHAMA kutoka nchi za Bonde la Ufa wakimsikiliza Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa (hayupo pichani) akifungua mkutano wa siku mbili wa wadau Teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA) kutoka nchi za ukanda wa Bonde la ufa leo jijini Dar es salaam.
06
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa (katikati) akisalimiana na baadhi ya washiriki mara baada ya ufunguzi wa mkutano wa wadau Teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA) kutoka nchi za ukanda wa Bonde la ufa leo jijini Dar es salaam.(Picha zote na Eleuteri Mangi MAELEZO).

Post a Comment

Previous Post Next Post