YANGA YAMBAMIZA KAGERA BAO 2 - 1

Wachezaji wa Yanga, wakishangilia bao la pili lililofungwa na Didier Kavumbagu (pichani wa pili kushoto) katika dakika ya 34 ya kipindi cha kwanza, huku bao la kwanza likifungwa na Hamis Kiiza katika dakika ya 3, mabao yaliyodumu hadi mwisho wa mcheo huo. 
Bao la kufutia machozi la Kagera Sugar, lilifungwa na Daud Jumanne, katika dakika ya 63 baada ya beki wa Yanga Oscar Joshua, kujaribu kumrudishia kipa wake mpira wa kichwa uliokuwa mfupi na kunaswa na mshambuliaji huyo aliyemchambua kipa wa Yanga, Deogratias Minishi. 
Hadi mwisho wa mchezo huo Yanga ya Jijini Dar es Salaam, 2 na Kagera Sugar ya Mjini Bukoba 1. Na katika habari kutoka Mlandizi zinasema kuwa mchezo kati ya Azam Fc na Ruvu Shooting, umeahirishwa kutokana na Uwanja wa Mlandizi Mabatini kujaa maji kutokana na mvua iliyonyesha leo, na mchezo huo sasa unatarajiwa kuchezwa kesho.
Mabeki wa Kagera Sugar, akimdhibiti Simon Msuva.
Didier Kavumbagu, akitunishiana msuli na wachezaji wa Kagera Sugar.
Hii si Sarakasi bali ni moja kati ya staili ya kuokoa hatari....
Hapa si kwamba wanacheza Bruzi, bali ni beki wa Kagera Sugar akijaribu kumdhibiti mshambuliaji wa Yanga, Didier Kavumbagu.
Sio kwamba ni staili ya kwenda mpaka chini, bali hapa beki wa Kagera Sugar, akiendelea kumdhibiti Kavumbagu.
Simon Msuva, akijiandaa kupiga Krosi.
Didier Kavumbagu (kulia) akimfinya beki wa Kagera Sugar.
Sehemu ya mashabiki wa Yanga.
Hussein Javu, akimburuza beki wa Kagera Sugar.

Post a Comment

Previous Post Next Post