Na Cleophus Tres Thomas III, Nairobi na Fuad Ahmed, Mogadishu
Wakati kikundi cha Kiislamu cha Nigeria cha Boko Haram kilipoteka nyara
wasichana wa shule 276 mwezi uliopita, kilipeleka wimbi la mshtuo
ulimwenguni kote na kulaumiwa katika sehemu kubwa.

Picha ya video iliyohifadhiwa katika picha
za kawaida iliyochukuliwa tarehe 12 Mei, 2014, kutoka kwenye video ya
kikundi cha Kiislamu cha Nigeria cha Boko Haram inaonyesha wasichana wa
shule waliotekwa wakiwa wamevaa hijabu ndefu na kushikilia bendera
inayohusishwa na Uislamu wa siasa kali. Boko Haram imechukua ukurasa
kutoka kwenye kitabu cha michezo cha al-Shabaab, wakidai katika video
hiyo kuwa wasichana hao wamebadilishwa kuwa Waislamu na kuonyesha
wakirudiarudia swala. [AFP PHOTO / BOKO HARAM]
Utekaji nyara wa tarehe 14 Aprili katika mji wa Chibok wa Nigeria hata
hivyo ulihamasisha lawama kali na kutoafikiwa na kikundi shirika chenzao
cha al-Qaeda. Lakini tukio hilo limeungwa mkono na kikundi kimoja:
kutoka kwa al-Shabaab.
Al-Shabaab, ambayo pia ina desturi ya utekaji watoto kwa kutumia nguvu
na kuwaingiza jeshini kupigana, ilitoa sauti ya kuunga mkono kitendo cha
kikundi cha Nigeria kupitia ukurasa wa Facebook wa Redio al-Andalus.
Katika mfulululizo wa taarifa kuanzia tarehe 10 Mei, al-Shabaab ilihoji
kwamba utekaji huo umehalalishwa kama matokeo ya unyanyasaji wa serikali
ya Nigeria dhidi ya Waislamu na kwamba Boko Haram "iliwaokoa" wasichana
hao wadogo kutoka kwenye ukatili huo.

Maofisa wa polisi wakipitapita katika
shule hiyo katika mji wa Chibok wa Nigeria ambako wasichana wa shule
zaidi ya 200 walitekwa nyara na Boko Haram tarehe 21 Aprili, 2014. [AFP
PHOTO / STR]
Kama majaribio ya awali ya hoja hii, al-Shabaab katika taarifa yake moja
inaonyesha mfululizo wa picha ambazo ilidai ni askari polisi wa Nigeria
wanaowalazimisha Waislamu majeruhi au walemavu chini wakati ofisa
"Mkiristo mdogo" anaonekana kutekeleza mauaji. Taarifa hiyo pia
ilionyesha kwamba Waislamu wanapaswa kohoji dhidi ya vitendo hivi na
"kumwaga damu" kulipa kisasi.
Al-Shabaab pia ilijaribu kuhalalisha kitendo cha Boko Haram ikisema ni
ya kiasi kidogo cha unyanyasaji wa kibinadamu ukilinganishwa na utendaji
mbaya wa serikali kwa Waislamu walio katika magereza za Nigeria.
"Mujahidina wanawatendea wanawake kwa heshima," moja kati ya matamko
katika ukurasa wa Facebook wa al-Andalu ulieleza. "[Kila msichana]
atapewa mwanaume mmoja ambaye atamfanya kuwa mke wake au kumuuza kwa
mwanaume mwingine anayemtaka. Baadaye, wataachiwa huru na kuolewa kama
wanawake [wengine] walio huru."

Picha ya video iliyohifadhiwa katika picha
za kawaida iliyochukuliwa tarehe 12 Mei, 2014, kutoka kwenye video
iliyotolewa na Boko Haram inamwonyesha mwanaume anayedaiwa kuwa kiongozi
wa kikundi hicho Abubakar Shekau. [AFP PHOTO / BOKO HARAM]
Katika taarifa nyingine zilizotumwa, al-Shabaab waliwataka wafuasi wao
kupaza sauti kuhusu majaliwa ya wasichana waliotekwa, wakitoa matukio
matatau:
1. Je, wanaweza kuachiwa bila ya masharti?
2. Je, wanaweza kuachiwa huru kwa kulipa fidia?
3. Je, wanaweza kutolewa kwa majihadi wengine ili wavulana 200 zaidi waweze kuzaliwa ili kujiunga na mujahidina?
Taarifa zilizotumwa zilidai kwamba uchaguzi wa aina tatu unaruhusiwa
chini ya sharia kama wasichana watachukuliwa kama sehemu ya "makafiri"
au "wasioamini".
Majibu ya wasomaji yaligawanywa kati ya uchaguzi 1 na 3 -- kuwaachia
wasichana bila ya masharti na "kuwatoa" kwa mujahidina ili kusaidia
kuundwa kwa jihad.
"Nafikiri wangeachiwa bila ya masharti. Wanazuoni wa Kiislamu wamekubali
kwa asilimia 100 kwamba utekaji ni makosa," msomaji mmoja alisema,
akiongeza kwamba kuwateka wasio Waislamu wanaoishi kwa amani na Waislamu
kutaharibu sifa ya Uislamu.
Wengine walililaumu kundi kwa jumla.
"Kuna viwango vya jihad. Boko Haram hawakupata hata neno zuri kutoka kwa
wanazuoni wa jihadi au al-Qaeda. Vitendo vyao ni dhambi na hawana elimu
ya kutosha ya Uislamu," msomaji mwingine alituma.
"Al-Andalus, msiwapotoshe watu. Wanamgambo sio mujahidina," alisema. "Ni
kweli kwamba Waislamu wananyanyaswa na kuuawa, lakini walichokifanya
[Boko Haram] ni kitu ambacho hakiwezi kuvumiliwa."
"[Boko Haram] sio mujahidina; ni mashetani," msomaji mwingine aliandika.
"Wanakosea na sharia ya kiislamu hairuhusu kuoa wanawake kwa
kuwalazimisha. Ninaomba kwa Mungu wawaachie wanawake waliowatorosha."
Wasomali walaumu msaada wa al-Shabaab kwa Boko Haram
Sheikh Said Sheikh Mohamud Sheikh Abdirahman, mkuu wa masuala ya haki wa
Ahlu Sunna wal Jamaa huko Guriel, alisema yeyote mwenye elimu ya kweli
ya Uislamu anajua kwamba utekaji nyara wa wasichana uliofanywa na
hauruhusiwi.
"Uislamu umempa binadamu heshima maalumu, hasa [kwa] wanawake ambao haki
zao lazima zilindwe," aliiambia Sabahi. "Kwa hiyo, unafikiri [Uislamu
unasema nini] kwa mtu anayewatorosha wasichana wadogo wanaokwenda shule,
hata kama sababu ya kuwatorosha ni kutaka au kutotaka fedha, au kwa
sababu za kisiasa?"
"Kila Muislamu anaelewa na hakuna maswali kuhusu uharamu wa utoroshaji," alisema.
"Wanaume wanaofanya utekaji wa namna hiyo ni watenda dhambi [wabaya
sana] kuliko ambavyo tumeona kabla," alisema. "[Hili] ni jambo la kuonea
aibu kwa kila namna."
Abdirahman alisema hakushangaa kwamba vituo vya habari vya al-Shabaab vinasifia vitendo vya makundi mengine ya magaidi.
"Ni kitu kinachotarajiwa katika kikundi, ambapo ukataji vichwa na mabomu
ya kujitoa muhanga ni vitu vya kawaida, kushangilia utekaji nyara wa
kundi la ugaidi pamoja na itikadi zinazofanana," alisema, akiongeza
al-Shabaab wamekuwa wakihusika na hata uhalifu mkubwa kuliko
wanachokifanya Boko Haram sasa.
Hassan Ali, mzee wa mila mwenye miaka 53 kutoka Mogadishu, alisema
al-Shabaab na Boko Haram ni vikundi vyenye tabia zinazofanana.
"Wakati vikundi vya magaidi vinavyofanana na al-Shabaab, ambavyo
vimeibuka vikali katika miaka kumi iliyopita duniani kote na katika nchi
za Afrika, vimedhoofishwa, wengi wanateka na kufanya unyanyasaji dhidi
ya watoto na wanawake," Ali aliiambia Sabahi.
"Ndiyo sababu nilikuwa na huzuni sana niliposikia kundi la Boko Haram
liliwateka wanafunzi wasichana," alisema. "Imenikumbusha vitendo
walivyovifanya al-Shabaab katika miji mingi nchini Somalia
walipoyadhibiti."
#RejesheniWasichanaWetu
Utekaji wa wanafunzi wa kike umesababisha kelele na kuchochea kampeni za
mitandao ya kijamii duniani kwa kutumia mitandao ya kijamii --
#RejesheniWasichanaWetu.
Viongozi wa serikali ya Marekani siku ya Alhamisi (tarehe 15 Mei)
walikosoa vikali hatua za "taratibu" dhidi ya utekaji na vitisho vya
Boko Haram kwa ujumla.
Mwenyekiti wa Kamati ya Seneti wa Uhusiano wa Kigeni Robert Menendez
alisema Nigeria imekuwa "nzito sana mpaka inakuwa sikitiko na
hakikubaliki" namna inayoshughulikia mgogoro, pamoja na kupata msaada
kutoka Marekani na nchi nyingine.
"Nimetoa wito kwa Rais [Goodluck] Jonathan kuonyesha uongozi ambao taifa lake linahitaji," alisema Menendez.
"Katika sura ya tishio hili lenye utata, vikosi vya usalama vya Nigeria
vimekuwa taratibu kufuata mikakati na mbinu mpya," alisema kiongozi wa
Idara ya Ulinzi ya Marekani Alice Friend.
Nchi ya Marekani imepeleka timu ya raia na wataalamu wa jeshi 30
kusaidia serikali ya Nigeria kuwasaka wasichana wanafunzi waliotekwa.
Jeshi la Marekani limekiri kurusha ndege zisizokuwa na marubani pamoja
na ndege za uchunguzi zenye watu nchi nzima katika jitihada za
kuwatafuta wasichana hao.
Asha Farah, mwenye umri wa miaka 26 aliyesoma utawala wa umma katika
Chuo Kikuu cha Mogadishu, alikaribisha msaada uliotolewa na serikali ya
Marekani na jumuiya ya kimataifa katika kuwatafuta wasichana
waliotoroshwa na Boko Haram.
"Ninakiona hiki kama kitendo kibaya sana kilichofanywa na kikundi cha
Boko Haram, ambacho kinadai kuwa kikundi kinachopigana kwa jina la
Uislamu. Hiki ni kitendo ambacho magaidi wa kimataifa wanajulikana
kukifanya," alisema.
"Katika kuunga mkono ombi lililotolewa na wazazi wa Nigeria, ninawaomba
Boko Haram kuwaachia watoto kama wanajali kuhusu ubinadamu hata chembe,"
alisema.
Chanzo: sabahionline.com
Post a Comment