Angelina Jolie hataki wanae wawe waigizaji kama yeye na baba yao, Brad Pitt. Muigizaji huyo mrembo anataka waje kuwa wanasiasa.

Jolie mwenye miaka 38, ana watoto sita na mchumba wake wa siku
nyingi Brad Pitt, 50, lakini alikiri kuwa anatumaini watafuata ndoto
zingine tofauti na kuigiza. “Najaribu kuwavutia kwenye siasa. Wanangu wa
kiume na w kike wanaweza kuwa na kazi zingine kubwa badala
yake,”alisema.
Wapenzi hao husafiri na watoto wao wa kiume Maddox, 12, Pax, 10, na
Knox, 5 pamoja na wa kike Zahara, 8, Shiloh, 6 na Vivienne, 5 wakati
wakipromote filamu zao duniani kote lakini anadai kuwa anapenda waone
pia sughuli za kibinadamu. Akiongea na gazeti la The Sun aisema:
“Wanajua tunatengeneza filamu. Lakini pia kuwa baba yao hutengeneza
samani na kujenga nyumba na kwamba mama anapenda kusafiri na umoja wa
mataifa.”
Hata hivyo Angelina amewahi kumtumia mwanae wa kike Vivienne, kwenye
filamu yake mpya ‘Maleficent’, wakidai kuwa wanae wengine walikuwa
wakiogopa nguo zake.

Post a Comment