BAADA YA TAARIFA KUENEA KUWA STAA WA FILAMU ZA KIBONGO,WEMA SEPETU ANAUMWA,MSANII HUYO AMEFUNGUKA KINACHOMSUMBUA - Msikileze/Soma Hapa

 
Wiki hii haikuwa poa kwa mastaa wa Bongo ambapo alianza msanii Shaa kupigwa na malaria siku ya tuzo za Killi zilizofanyika katika ukumbi wa Mlimani City,ambapo alishindwa kupafomu.Jumapili hii msanii wa bongo fleva Rehema Chalamila ‘Ray C’ alipatwa na homa ya Dengue mpaka akalazwa hospitali ya Mwananyamala na sasa anaendelea vizuri na amesharuhusiwa hospitalini, akafuatia msanii wa Bongo Movie Muhsin Awadh ‘Dr Cheni’ naye alipatwa na homa hiyo ya dengue.Siku za hivi karibuni taarifa zilienea kuwa staa wa filamu za Kibongo,Wema Sepetu anaumwa,msanii huyo amefunguka kinachomsumbua na kusema kuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa malaria.
 
 

Chanzo:-  cloudsfm

Post a Comment

Previous Post Next Post