Benki ya NMB yazindua kampeni ya Jihudumie .


Benki ya NMB imezindua kampeni mpya ya Jihudumie yenye lengo la kuwezesha upatikanaji wa haraka wa huduma mbalimbali za benki hiyo. Akizindua kampeni hiyo jijini Dar es Salaam Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB, Bw. Mark Wiessing alisema mbali ya upatikanaji wa huduma haraka, kampeni hiyo itawezesha huduma kupatikana muda wowote na mahali popote.
sinza mbogela Afisa Mkuu wa Ukaguzi wa ndani wa benki ya NMB Bw. Augustino Mbogella (Kulia) akielimisha wateja katika tawi la NMB Sinza kuhusu huduma za jihudumie ambazo ni, NMB mobile, PesaFasta, NMB ATM, NMB ChapChap account, POS, NMB Tigo Pesa, NMB M-Pesa na NMB inakubalika hapa

Sasa wateja wa NMB wanaweza kupata huduma bila kwenda katika tawi la NMB. “Tunapenda kuwafahamisha wateja wetu kwamba sasa wanaweza kupata huduma za kibenki kupitia simu za mkononi na njia nyingine mbadala kama mashine za ATM, huduma za benki kwa njia ya intaneti, PesaFasta na Akaunti ya Chap Chap,” alisema Wiessing.
Kariakoo Afisa Mkuu wa Fedha wa benki ya NMB Waziri Barnabas (kushoto) akimpa maelekezo ya kutumia huduma ya kifedha ya Jihudumie Frances Mbena katika tawi la Kariakoo Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo
Kupitia kampeni hiyo, NMB imeweza kuzingatia mahitaji ya msingi ya wateja wake, ikiwemo uhakika wa huduma za kibenki na uwezo wa kuzipata wakati wowote na mahala popote. “Kwa kubonyeza tu kitufe cha simu, fedha itaweza kutoka kwenye akaunti yako ya NMB kwenda mahala pengine popote kama vile kwenye malipo ya LUKU, kulipia muda wa maongezi wa simu na hata kuweza kutoa kiasi kinachofikia shilingi milioni moja kupitia mashine za ATM,” alisema.
makungwa-magomeni Afisa Mkuu wa Huduma kwa Wateja Wakubwa wa NMB Richard Makungwa akiwapa maelezo wateja kuhusu huduma wa Jihudumie katika tawi la NMB Magomeni
Baada ya uzinduzi huo mwendelezo ulifanywa kwa matawi yote ya benki hiyo jijini Dar es Salaam, wateja wa benki hiyo walisifia kampeni hiyo, wakisema imelenga kuwapunguzia adha, usumbufu na kuokoa muda wa kupata huduma za kibenki.
NMB
Afisa Mkuu Operesheni na Mawasiliano wa NMB Pete Novat (kulia) akimwelekeza mteja katika tawi la NMB Temeke jinsi ya kujisajili na huduma ya NMB mobile kupitia mashine ya ATM

Post a Comment

Previous Post Next Post