Ukweli ni kwamba kwa
sasa mavazi ya yaliyotengebezwa na material za kiAfrika aka “African
Prints” ndio yanaopendwa zaidi na Bibie Beyonce amekua kati ya miongoni
mwa wasanii ambao wanapenda sana, Beyonce alianza kuvaa mavazi haya
kutoka kwa designer Mtanzania aishie nchini uongereza ajulikanae kwa
jina CHICHIA LONDON katika moja ya concert yake akiwa ndani ya Hot Pant
ya designer huyo. Mavazi yanayotengenezwa kwa Batiki, Vitenge, Khanga na
material mengine yenye asili ya Afrika yametokea kukubalika sana
dubiani kwa sasa, Tumeshuhudia baadhi ya wasanii wakubwa wakivaa batiki
na kupendeza huku miaka michache iliyopita kijana akionekana kavaa
batiki ilionekana ni ushamba.
Beyonce ni mmoja wa wasanii wachache kabisa kutoka Marekani ambao
wameonekana mara nyingi wakiwa wamevaa nguo zenye asili ya Afrika.
Alishawahi kuvaa nguo iliyotengenezwa kwa kitenge, akafanya show huku
akiwa amevaa nguo iliyotengenezwa kwa khanga tena yenye maneno ya
kiswahili na zamu hii kaja na viatu vilivyotengenezwa kwa kitenge.
Unaweza tazama picha za Beyonce akiwa katokelezea kiafrica zaidi hapa chini.
Post a Comment