
Baadhi
ya wakazi wa Tandika sokoni jijini Dar es Salaam,wakisoma vipeperushi
vyenye ujumbe wa “Fistula inatibia” wakati wa kampeni ya kutoa elimu kwa
Umma juu ya tatizo hilo kuwa linatibika kwa ushirikiano wa wadau wa
CCBRT,UNFPA na Vodacom Foundation.Kampeni hizo zinafanyika nchi nzima
katika kuaziamisha siku ya Fistula duniani.
Katika
maadhimisho ya pili ya siku ya kutokomeza fistula ya uzazi duniani,
mabalozi 100 wa kijamii wataendesha warsha za wazi kueneza ujumbe
“Fistula Inatibika”
Leo
Mei 23, 2014 mabalozi 100 wa CCBRT wataendesha mafunzo ya wazi sehemu
mbalimbali nchini yenye lengo la kuzijengea jamii uelewa kuhusu fistula
na kuwataka wanawake wenye matatizo hayo kujitokeza kupata matibabu.
Wiki iliyopita, mabalozi 100 kutoka mikoa 25 Tanzania walihudhuria
mafunzo ya namna bora ya kuendesha simian hizo za kijamii kwa mafanikio
pamoja na kuwezeshwa vifaa vya kazi tayari leo kwa sauti moja
iliyoungana watu hao 100 wanasambaza ujumbe wa “Fistula inatibika.”
Juhudi
hizi ni matokeo ya ushirikiano kati ya CCBRT na wadau wake ambao wote
kwa pamoja wameweka azima ya dhati ya kupambana na fistula na kumaliza
tatizo hilo hapa nchini.
Akizungumza
jijini Dar es salaam, Ofisa Mtendaji Mkuu wa CCBRT Erwin Telemans
alisema “ Maelfu ya wanawake sehemu mbalimbali hapa nchini wanaishi
maisha ya aibu na kutengwa kutokana na kusumbuliwa na fistula bila
kufahamu kwamba CCBRT na wabia wake wanatoa matibabu bure ikiwa ni
pamoja na kubeba gharama zote za usafiri wa wagonjwa kufika Dar es
salaam,malazi na chakula. Mabalozi wetu wa kijamii wapo katika nafasi
nzuri ya kuwafikia wanawake hao na kimisingi katika kipindi cha mwaka
mzima wamekuwa wakifanya kazi nzuri ya kuwafikisha kwetu wanawame hao
kwa matibabu. Leo tunawaomba wachukue hatua za ziada na tunaimani kuwa
wakiwa na nguvu mpya katika mikakati yetu ya kueneza ufahamu kwa jamii
kuhusu fistula watawashawishi wanawake wengi zaidi kutoka mafichoni.”

Mmoja
wa wasanii wa kundi la “Mpoto Theater”akigawa vipeperushi kwa Mariam
Khamis vyenye ujumbe wa “Fistula inatibia” wakati wa kampeni ya kutoa
elimu kwa Umma juu ya tatizo hilo kuwa linatibika kwa ushirikiano wa
wadau wa CCBRT,UNFPA na Vodacom Foundation.Kampeni hizo zinafanyika nchi
nzima katika kuaziamisha siku ya Fistula duniani.
Mtandao
wa mabalozi wa CCBRT hutumika kuwabaini na hatimae kuwasafirisha
wanawake wenye tatizo la fistula kwa ajili ya matibabu. Pindi balozi wa
fistula anapombainisha na kumthibitisha mgonjwa hufanya mawasiliano na
CCBRT kupitia nambari maalum ambayo ni bure kwa wateja wote wa Vodacom
na baada ya hapo CCBRT hufanya utaratibu wa kutuma fefha za nauli
zinazotumwa kwa njia ya M-pesa na hapo mwanamke mwenye fistula huanza
safri kuelekea CCBRT Dar es salaam au kwenye moja ya hospitali
zinazofanya nazo kazi ya Kigoma, Arusha na Moshi.
Kwa
kila mgonjwa mmoja anaefikishwa hopsitali balozi wa CCBRT hupata Sh
10,000/- kama motisha kwa kusaidia kumaliza tatizo la fistula Tanzania.
Kwa
sasa mtandao wa mabalozi wa fistula unafikia mabalozi 500 wanaofanya
akzi kwa utaratibu w akujitolea wakifikisha hopsitali wagonjwa wapatao
2,000
“Kutumika
kwa tekonolojia ya Vodacom kumesaidia kupunguza vikwazo kwa wanawake
wanaotafuta matibabu na ni moja kati ya ubunifu mkubwa kwenye sekta ya
afya kuwahi kushuhudiwa hapa Tanzania. Urahis wa kutumia huduma za
kifedha za simu ya mkononi umeokoa heshima ya maelfu ya wanawake walio
masikini na waliotengwa hapa nchini kwa sababu tu ya fistula. “Alisema
Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Bw Rene Meza na kuongeza

Kikundi
cha wasanii wa muziki wa kiasili cha “Mpoto Theater”wakitumbuiza na
kuonesha vipeperushi vyenye ujumbe wa “Fistula inatibia” wakati wa
kampeni ya kutoa elimu kwa Umma juu ya tatizo hilo kuwa linatibika.
Kampeni hizo zinafanyika nchi nzima katika kuaziamisha siku ya Fistula
duniani,zilizoandaliwa na CCBRT,UNFPA na Vodacom Foundation.
“Ubia
wa Vodacom Foundation na CCBRT umekuwa ukiimarika siku hadi siku na
tunajivunia kufanya kazi na wabia wetu mahiri katika kuadhimisha siku
moja ya juhudi zetu pana za kumalzia fistula hapa nchini.”
Siku
ya kimataifa ya kutokomeza fistula huadhimishwa Mei 23 ya kila mwaka
kutambua umuhimu wa juhudi za kumaliza tatizo hilo na pia kuonesha nia
ya dhati ya Umoja wa Mataifa kwa juhudi zote zinazofanywa za kutibu na
kukinga fistula duniani.
“Kama
sehemu ya jamii, tunawajibu wa kumaliza janga hili la kiafya na kiutu,
Tunavyoadhimisha siku hii leo, wote lazima tukubaliane kwamba kumaliza
fistula hakuhsu tu upasuaji kwa mgonjwa. Ukweli wa mambo ni kwamba
tunaweza kumaliza tatizo hili nchini kwa kuwekeza kimkakati kwenye
maeneo matatu ambayo ni kinga, matibabu na kuwarejesha katika maisha ya
awali ya kijamii wale waliowahi kuugua na kupona.
Una
mtu mwenye fistula? Ungependa kuwa balozi wa CCBRT? Piga CCBRT (bure
kwa wateja wote wa Vodacom) ili kupata taarifa zaidi au kumfikisha
hospitalikwa ajili ya matibabu mwanamke anaegua fistula 0800752227

Wakazi
wa Mbagala mwisho jijini Dar es Salaam Bi.Fatuma Ali(kushoto)na Khadija
Rajabu wakiwa wakionesha vipeperushi vyenye ujumbe wa “Fistula
inatibia” wakati wa kampeni ya kutoa elimu kwa Umma juu ya tatizo hilo
kuwa linatibika. Kampeni hizo zinafanyika nchi nzima katika kuaziamisha
siku ya Fistula duniani na ratibiwa na CCBRT,UNFPA na Vodacom
Foundation.

Msaani
wa muziki wa kugani Mrisho Mpoto akitoa elimu kwa wakazi wa Mbagala
rangi tatu kwa njia ya kugawa vipeperushi vyenye ujumbe wa “Fistula
inatibia” wakati wa kampeni ya kutoa elimu kwa Umma juu ya tatizo hilo
kuwa linatibika. Kampeni hizo zinafanyika nchi nzima katika kuaziamisha
siku ya Fistula duniani na ratibiwa na CCBRT,UNFPA na Vodacom
Foundation.

Wafanyabiashara
ndogondogo wa Mbagala rangi tatu jijini Dar es Salaam Abdalla
Juma(kushoto) Albart Mhogo(kulia)wakisoma vipeperushi vyenye ujumbe wa
“Fistula inatibia” wakati wa kampeni ya kutoa elimu kwa Umma juu ya
tatizo hilo kuwa linatibika. Kampeni hizo zinafanyika nchi nzima katika
kuaziamisha siku ya Fistula duniani na ratibiwa na CCBRT,UNFPA na
Vodacom Foundation.
Post a Comment