Chege |
Msanii wa muziki kutoka pande za TMK, Chege Chigunda amesema
kuwa ameshamaliza kurekodi wimbo wake mpya uitwao ‘Wauwe’ na yupo
kwenye mchakato wa kuanza kushoot video yake na director mkongwe Adam
Juma.
Chege ameiambia Bongo5 kuwa anaamini kuwa Adam Juma atafanya mambo makubwa katika kazi hiyo itakayotoka baada tu ya kumalizika.
“Kwanza wimbo wangu umefanywa na maprodyuza wawili,Sheddy lever na
Marco Chali, kwahiyo audio iko tayari natarajia kushoot video weekend
ijayo na Adam Juma halafu itatoka. Mimi nafanya video zangu na Adam Juma
because I believe Adam Juma na nitaendelea kufanya na Adam Juma mpaka
nione mwisho wake. Kufanya nje ya nchi siyo solution ya kufanya kitu
kizuri,kufanya kitu kizuri anaweza akafanya mtu yoyote na kama ingekuwa
kufanya kitu kizuri ni nje basi wasanii wa ndani tusingefanya kitu.
Kwahiyo mimi nitaendelea kufanya naye mpaka mwisho wake nione kitakuwa
nini.”
Chege amedai kuwa ‘Wauwe’ ni ngoma ya party.
Post a Comment