Dogo Janja asema “Kwani Pancho Demu wangu akataze nisitoe Ngoma?, Asinitishe”

20140507-141129.jpg
 Baada ya ntafaruku wa kichini chini unaoendelea kati ya ‘Dogo JANJA’ na ‘Pancho LATINO’ kuhusiana na nyimbo mpya ambayo Dogo Janja yupo mbioni kuitoa kama single yake mpya ifuatayo mwaka huu 2014 na mipango ya kufanya video ipo mbioni Jumatatu ijayo.
Kwa mujibu wa Dogo Janja hiyo nyimbo yeye aliirekodi kwa producer Pancho ambayo amekua akiifuatilia kwa muda mrefu sana ili iweze kutoka lakini alichokua akikipata ni kitendo ambacho yeye alikiita “Mizinguo” ambayo Producer Pancho analeta kutaka kuchelewesha mipango ya wasanii, Janjaro alisema yeye alianza kumfuatilia pancho toka mwaka jana 2013 mpaka leo. Kwa mujibu wa Dogo Janja yeye baada kuona mizinguo hiyo ikiendelea na sababu nyimbo aliiandika yeye, aliamua kuachana na ngoma hiyo kwa Pancho wa BHitz na kufunga safari na kwenda kwa producer ‘DX’ mjini Arusha na kuirekodi tena nyimbo hiyo kwa kutumia Beat nyingine kabisa.
Baada ya kitendo chake kwenda kufanya kazi kwa DX, Pancho kusikia kionjo tu cha nyimbo hiyo, alimpigia simu DX na kumwambia kuwa asije akasikia ameachia nyimbo hiyo sababu yeye ana haki na nyimbo hiyo na imeshafanyika kwake na akijaribu kutoa na yeye atalikisha ile ambayo yeye ameshaifanya kama kawaida ya tabia ya STUDIO hiyo ya BHitz kuwafanyia wasanii waliotoka hapo kama walivyofanya kwa Mabeste na Mrap Lion. Akizungumza kwa uchungu sana Janjaro alisema…
“Pancho mie sio ‘Demu Wangu” akataze nyimbo yangu kutoka wakati mistari nimeiandika mwenyewe… Amenisumbua zaidi ya miezi saba natoka ubungo kwenda studio halafu hapokei simu zangu… Mie ni msanii siwezi kupanda daladala ila nahangaika mpaka natumia boda boda kuweza kufika studio sababu yeye aliniambia kuwa ‘Hermy B’ amesema ile ni nyimbo ambayo natakiwa kuitoa halafu unampigia simu ukamalizie ngoma anakua mjinga kuacha kupokea simu zangu…” Alisema Janjaro akihojiwa kwa njia ya simu na GongaMX Media moja kwa Moja mchana huu kutoka Arusha.
Janjaro aliongeza kuwa yeye atanyayasika na maproducer Dar lakini sio Arusha…. “Mwambie huyo Pancho sijatumia beat yake na yeye ataninyanyasa Dar lakini nikiwa Chuga kaka zangu wananifata nyumbani wanaenda kunipeleka Studio nafanya ngoma kwenye Beat kali na narudishwa nyumbani…. Mie hii ngoma naitoa muda si mrefu na Pancho hawezi kunifanya chochote tena asiniudhi kabisa na mambo yake ya ajabu ajabu” aliongeza JANJARO.
Pancho alipigiwa simu na kuambiwa issue nzima na malalamiko kutoka kwa Janjaro na yeye alisema kuwa hajui swala la nyimbo hiyo na wala hajui issue hiyo iko vipi na amekataa kuwa hajampigia simu DX na kuwa DX ndio alimpigia simu yeye, Pancho Latino aliahidi kutuma whatsapp message ambazo alikua anachat na Janjaro kuhusiana na nyimbo hiyo ambayo mwanzoni alikataa kuwa hajui issue youote kuhusu nyimbo hiyo.
BHitz ni Label ambayo imekua na mtafaruku na wasanii wengi sana kwa muda mfupi sana na kusababisha jopo zima kali la BHitz Music Group kuondoka, na hii ni kuanzia mwanzo ambapo wasanii kama AY na Mwana FA waliondoka kutoka na urasimu huo, vile vile bila kusahau wasanii ambao wapo kwenye game kwa sasa kama Vennesa MDEE, Mrap Lion, Gosby, Mabeste na Deddy ambao walikua na mkataba nao lakini kinachosemekana kutoka kwa wasanii wote hawa ni Producer Pancho Latino ndio mwenye matatizo kuliko maboss wao.

Post a Comment

Previous Post Next Post