Rapper Fareed Kubanda aka Fid Q amesema ameangalia udhaifu alionao kwenye muziki wake na amegundua kuwa huwa hana video kali.
Akiongea leo kwenye kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio,
Fid amesema mashabiki wake wategemee video kali kutoka kwake ili
kuuondoa udhaifu huo.
Katika hatua nyingine, Fid Q amesema amewainspire 95% ya rappers wa Tanzania ndio maana anajiamini.
“Katika hip hop kuna mambo mengi, kuna suala linaitwa industry
impact, kazi zako zikoje tangu ‘Huyu na Yule’ akina Dot.com vitu
vimeendelea, zimekuja Mwanza Mwanza, Binti Malkia, August 13 mpaka leo
tupo katika ‘Siri ya Mchezo’,” amesema.
Fid ambaye mwaka huu ameshinda tuzo mbili za KTMA, amesema pia suala
jingine ni uwezo wa kubadilika ‘versatility’ kwenye nyimbo zake.
Post a Comment